Loading...

Thursday, January 25, 2018

Serikali yazifutia usajili kampuni tatu

Serikali yasitisha Shughuli za Kampuni Tatu (3) za Wakala binafsi wa huduma za ajira hapa nchini kutokana na kukiuka matakwa ya sheria ya huduma za ajira Na.9 ya mwaka 1999 na Kanuni zake.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi na wadau mbalimbali kuhusu utaratibu unaotumiwa na baadhi ya wakala binafsi wa huduma za ajira nchini.

Kampuni zilizofutiwa usajili baada ya kukiuka sheria ni pamoja na Sasy Solution Company Ltd, Bravo Job Centre Agency na Competitive Manpower International Ltd ambapo Kampuni hizo haziruhusiwi kujihusisha na shughuli za Uwakala  binafsi wa ajira  nchini.

Akifafanua Mhe. Mhagama amesema kuwa uchunguzi umebaini ukiukwaji wa taratibu za usajili ambapo baadhi ya mawakala wamekuwa wakitumia nyaraka zilizopatikana kwa njia isivyo halali katika kujipatia leseni za uwakala hali iliyowawezesha kukwepa kodi na kujipatia faida.

Aliongeza kuwa ukiukwaji wa taratibu za kisheria umeleta athari mbalimbali kwa wafanyakazi hasa kwa wale wanaoenda kufanya kazi Mataifa ya Nje ambapo wafanyakazi hao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ubaguzi na unyanyasaji katika ajira, malipo ya mishahara na stahiki mbalimbali.

Aidha, Mhe. Mhagama amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imesitisha mara moja shughuli za Mawakala Binafsi wa huduma za Ajira zinazohusika na kuwatafutia kazi wafanyakazi nje ya nchi (cross border placement) hadi hapo Serikali itakapoleta mfumo wa kusimamia jambo hili na kutoa taarifa kwa umma.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )