Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, January 29, 2018

VIDEO: Diamond Na Wema Walivyowapagawisha Mashabiki Ndani Ya Maisha Basement

Suprise ya nguvu imefanyika usiku wa kuamkia leo pale Hyatt Regency Hotel baada ya Malkia wa Bongo Movies, Wema Seetu kumpandisha mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz ukumbuni kwa ajili ya ufanya makamuzi.

Tukio hilo limetokea wakati wa hafla ya kumtambulisha msanii mpya wa Lebo ya WCB Wasafi, Mbosso ambaye amejiunga na lebo hiyo baada ya kundi lake la awali la Yamoto band kuvunjika.

Wakati sherehe ikiendelea, Rayvanny alikuwa akikamua, wakati akimalizia shoo alimuita Wema Sepetu ambaye aliibuka jukwaani kisha zikaanza kusikika kelele za mashabiki wakiimba …Wema…. Wema….Wema… ambaye baada tu ya kupanda na kuwasabahi mashabiki alimuita mpenzi wake wa zamani, Diamond Platinumz naye apande jukwaani.

Kelele ziliongezeka …Diamond… Diamond… Diamond…., haikuchukua muda Diamond akaibuka jukwaani na kukumbatiana na Wema kwa sekunde takribani 20 kabla ya kuanza kukamua.

Wakati Mond akikamua jukwaani na wasanii wengine wa WCB, Wema alikuwa akikata mauno jukwaani hapo jambo ambalo liliamsha msisimuko na shangwe miongoni mwa mwashabiki na kelele nyingi za kuwashangilia zikitawala.

Ikumbukwe kuwa Wema na Diamond waliwahi kuwa wapenzi miaka kadhaa iliyoita kabla ya kuachana na kila mtu kuingia kwenye mahusiano mengine.

Credit:GlobalPublisher
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )