Loading...

Monday, January 22, 2018

Waziri Mkuu ataka chama cha ushirika Mara kukaguliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itatuma wakaguzi ili wakague mali za Chama cha Ushirika cha mkoa wa Mara.

Amesema Serikali imeanza kufuatilia mali za vyama vya Ushirika nchini zikiwemo za chama cha Ushirika mkoa wa Mara.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumapili, Januari 21, 2018) katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Mara.

Alisema ukaguzi huo utakwenda sambamba na kufuatilia fedha wanazodai waliokuwa watumishi wa chama hicho.

“Kumekuwepo na matatizo makubwa ndani ya vyama vya ushirika kiasi cha kudumaza maendeleo ya wananchi.”

Pia Waziri Mkuu aliitaka mikoa yote ikomeshe matumizi ya vipimo visivyo rasmi kama butura na kangomba ili mkulima wapate tija.

“Vipimo hivyo ni vya kinyonyaji na vinamwibia mkulima na kuwanufaisha wafanyabiashara jambo ambalo si sahihi.”

Pia Waziri Mkuu aliziagiza Halmashauri zipunguze watumishi walio kwenye Makao Makuu ya Halmashauri na kuwapeleka maeneo ya vijijini ili wakawahudumie wananchi.

Alisema watumishi watakaobaki Makao makuu ya Halmashauri wanatakiwa nao waweke utaratibu wa usafiri ili kwenda vijijini kutatua kero za wananchi.

Kwa upande wa kilimo, aliagiza Maafisa Kilimo wote wapelekwe vijijini kuwahudumia wananchi na watakaobakia Ofisini ni Mkuu wa Idara, Afisa Bustani na Afisa Utafiti tu.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )