Monday, January 29, 2018

Zari amwambia Mama Diamond “Tuhame Guest House tumwachie mwanao”

Bado inaonekana swala la Diamond Platnumz kudaiwa kulala na wasichana wengine nyumbani kwake Madale, mama watoto wake Zari The Boss Lady hajaichukulia poa na inadaiwa kuwa amekasirishwa na tuhuma hizo zilizosambaa katika mitandao ya kijamii.

Diamond siku kadhaa zilizopita alidaiwa kupeleka msichana mwingine na kulala nae nyumbani kwake Madale, ila baada ya kuenea kwa video clip ikimuonesha msichana huyo akiwa Madale, Zari alionesha kukasirishwa na kuandika snapchat “Ati Madale State lodge au Madale Guest house?”
Baada ya siku kadhaa kupita baadhi ya mashabiki waliamini inawezekana swala hilo limepita ila comment ya Zari katika post ya instagram ya mama Diamond inaonesha amekasirika bado, hiyo ni baada ya ku-coment katika picha ya Mama Diamond aliyopost na kuandika “Kubwa la maadui” ikimuonesha Mama Diamond akiwa Madale lakini Zari akacomment “Fanya tuhame Guest House tumuachie mwanao”

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )