Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 23, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 05 na 06)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA   Kitendo cha kufunga mlango kwa funguo, nikamuwahi Maria kwa nyuma na kumshika kino, kwa haraka Mariam akakurupuka mikononi mwangu na kunigeukia. Akanitandika kofi moja zito la shavu huku akiachia msunyo mkali na mzito.

“Mimi sio malaya wa kujirahisha kwa mwanaume, na sijakuja hapa unitomb*, lala zako kitandani mimi nitalala hapa kwenye kochi”

Mariam alizungumza huku akiwa amekunja sura, akapiga hatua hadi lilipo sofa akajirusha na kukaa, huku akinikazia macho makali.

ENDELEA  
Sikuamini kwamba Mariam anaweza kuwa mkali sana kwenye hili. Kwa mtazamo wa haraka haraka ukimtazama unaweza kusema kwamba ni msichana anaye jirahisisha sana katika kulitoa penzi lake. Moja kwa moja nikajitupa kitandani huku nikijisikia aibu sana kwa kitu ambacho nimekifanya kwa Mariam kwa maana sikuhitaji kuweza kukifanya kwa haraka.

Kwa msongamano wa mawazo mengi nikajikuta nikipitiwa na usingizi. Simu iliyopo mfukoni mwangu ikanistua kwa mlio wake nilio uweka katika mfumo wa mtetemesho(vibration).  Taratibu nikaitoa mfukoni na kuitazama nikiwa na mawenge ya usingizi sana na kukuta anaye piga simu ni K2.

“Haloo”

“Umeamkaje?”

“Salama tu”

Nilizungumza huku nikijinyanyua kitandani, moja kwa moja nikayatupia macho yangu kwenye sofa na kukuta Mariam akiwa hayupo. Kwa haraka nikanyanyuka kwenye kitanda huku simu yangu ikiwa kwenye sikio.

“Vipi umesha jiandaa kwenda kazini?”

“Ahaa ndio”

“Sawa, mimi ndio natoka, yaani hapa nina hamu na wewe, natamani nije hata kwako unipatie japo goli moja kisha twende kazini”

“Usijali luch tutaonana”

Nilizungumza huku niki nimefungua mlango wa bafuni na kumkuta pia Mariam hayupo. Nikatazama saa ya ukutani na kukuta ni saa kumi na mbili na nusu.

“Ok basi ngoja mimi nitangulie”

“Sawa”

Nikakata simu na kuirudisha mfukoni. Nikatoka chumbani na moja kwa moja nikaeleka katika barabara, nikamuita bodaboda wa pikipiki na kumuomba aniwahishe nyumbani kwa haraka. Akafanya hivyo, hadi ninafika snyumbani ni saa moja kasoro. Nikampa dereva pikipiki pesa yake. Kitendo cha kufika getini nikakutana na Mariam uso kwa uso akifungua geti akiwa amevalia tisheti ya chuo hicho cha ualimu huku akiwa ameshika mkobwa wake mdogo.

    Mariam akanitazama kwa jicho kali huku akisimama, akanipita na kuondoka zake, akapanda pikipiki niliyo kuja nayo. Nikaingia ndani na kukutana na mama Mariam kwenye kordo akitoka kuoga.

“Mambo Dany”

“Poa shikamooo mama”

“Marahaba”

Kutokana nimechelewa sana kazini, sikutaka hadithi na mama Mariam. Moja kwa moja nikaelekea chumbani kwangu nikafungua. Nikachukua taulo na kuelekea moja kwa moja bafuni. Haraka haraka nikaoga na kurudi chumbani kwangu na kumkuta mama Mariam akiwa amekaa kwenye sofa la chumbani kwangu huku akiwa  amevalia kanga moja iliyo lowana lowana maji na kuufanya mwili wake kushikana na kanga hiyo.


Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )