Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, February 5, 2018

Bashe Aichambua Serikali

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) amefunguka na kusema kuwa kwa twakimu mbalimbali ambazo zinatolewa na BoT zinaonyesha mambo hayapo sawa hivyo kuna haja kubwa kwa Serikali kupitia Waziri wa Fedha kubadili sera zake za kibajeti.

Bashe alisema hayo akiwa Bungeni na kudai takwimu mbalimbali kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mwaka 2011 mpaka Disemba 2017 zinaonyesha kuwa kuna mabadiliko makubwa na vitu kushuka kwa kasi kubwa.

"Umefika wakati kama nchi hasa Wizara yetu ya Fedha kukubali kubadili sera zake za kibajeti, nitatoa takwimu chache ambazo ukitazama takwimu hizi zinazoonekana kwenye taarifa za BoT kuanzia mwaka 2011 mpaka 2017, mzunguko wa fedha umeshuka kutoka asilimia 22% ya mwaka 211 mpaka asilimia 1.8% ya sasa hivi, ukiangalia export hasa ya mazao ya kilimo ambayo ndiyo yameajiri asilimia 70 Tanzania, ukichukua zao la Kahawa mwaka 2011 gross late yake ilikuwa asilimia 55% lakini sasa hivi ni asilimia -5.4, Cotton mwaka 2012 ilikuwa kwa asilimia 16% saizi imekuwa kwa asilimia - 3.8%, Sisal ndiyo imekuwa na ongezeko la asilimia 2.9 iliyokuwa mwaka 2012 saizi ipo kwa asilimia 4% .

"Manufacturing mwaka 2011 ilikuwa kwa asilimia 96% gross late sasa hivi imekuwa kwa asilimia -244, tafsiri yake ni ndogo tu sera zetu hazichochei ukuaji wa biashara na uchumi katika nchi. 

"Takwimu zinaonyesha Watanzania tunakuwa kwa wastani wa asilimia 2% na kitu lakini ukuajia wetu wa kilimo ni asilimia 0.4% hakuna uwiano hapa hili ni jambo ambalo hata tukasema humu dani ya Bunge lisifurahishe upande wa Serikali kwa kauli zetu lakini tunajukumu la kusema ukweli na ni muhimu kabisa Wizara ya Fedha ikakubali kwamba sera za kibajeti za Wizara ya Fedha siyo rafiki katika kuchochea kukuza uchumi wetu"  alisema Bashe
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )