Loading...

Friday, February 9, 2018

Habari Njema kutoka kwa Waziri Mwigulu kwa walionyang’anwa Pikipiki na Polisi

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina makosa madogo waziachie na wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.

Dk Mwigulu amesema yale yenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita, madawa ya kulevya, na wale wanaotelekeza wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka mahakamani au kuziteketeza na zenye makosa madogo wazitatue haraka na kuwarudishia na kuwapa elimu wamekosea wapi.

“Wapeni masomo wamekosea wapi, walekezeni na waliowabishi warekebisheni lakini tusirundike tukatengeza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake tunao, tutumie huu mkono wakutatua kwa yale ambayo yapo ndani ya mamlaka yetu” alisema Dk Mwigulu

Alisema kuwa ipo haja ya vijana sasa kufundishwa zaidi kuhusu sheria ya usalama barabarani ili kupunguza ajali ya pikipiki na mlundikano wa pikipiki katika vituo vya polisi nchini kwani kila napopita kita vituo vya polisi hukuta pikipiki ni nyingi na makosa yao ni madogomadogo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )