Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 15, 2018

Ilivyokuwa Kesi ya kujiunganishia Bomba la Mafuta ya Dizeli Nyumbani

adv1
Mfanyakazi Mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia (TAZAMA) Samwel Nyakirang’ani (63) na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa kujiunganishia Bomba la Mafuta ya Dizeli wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iwapatie dhamana.

Maombi hayo wameyawasilishwa kupitia Wakili wao, Kusalika Augustine mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo alidai wateja wake wanahitaji kupata dhamana kwa sababu mashtaka yanayowakabili yanadhaminika.

Kutokana na maombi hayo, upande wa mashtaka uliomba kesi hiyo iahirishwe ili wajibu hoja hizo, ambapo Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi February 22, 2018.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo  ni Nyangi Mataro ambaye ni Mwalimu wa Shule ya  msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni.

Wengine ni Mfanyabaishara, Farijia Ahmed, Malaki Mathia, Kristomsi Angelus, Pamfili Nkoronko na Hunry Fredrick.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali Bomba la Mafuta ya  Dizeli, kinyume cha sheria  ya Uhujumu uchumi.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )