Tuesday, February 27, 2018

Kamanda Mambosasa Amtaja Mtu Hatari Na Katili Sana Kwa Wanwawake

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Rajabu Mohamed(25) ambaye anatuhumiwa kujifanya Freemason na kisha kufanya kila aina ya ukatili kwa wananchi hasa wanawake.

 Akizungunza  jana,Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Sar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa mtu huyo amekuwa akifanya matukio hayo kwa muda mrefu na sasa wamefanikiwa kumkamata.

Mtuhumiwa huyo amedaiwa kuwa kwa muda mrefu amekuwa akifanya matukio ya kikatili kwa wanawake,kufanya unyang’anyi wa mali na kutoa vitisho kwa anaowafanyia ukatili huo kuwa wakitoa taarifa atawanyonya damu na kukata viungo vya sehemu za siri huku akiwafanya kila aina ya unyanyasaji wa kijinsia.

Mambosasa amesema kuwa baada ya kumhoji mtu huyo amekiri kufanya kila aina ya unyanyasaji ,kupora fedha,kuchukua kadi za benki na kutaka namba za siri,kufanya matukio ya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake.

“Huyu mtu tumemuhoji anasema kwa sasa ameacha,ukimuangalia sura yake ni ya binadamu lakini ni mnyama wa hali ya juu kabisa kama mnyama wa Seronera .Amefanya mambo mengi ya kishenzi.

” Tunaendelea na taratibu nyingine na baada ya hapo atapelekwa mahakamani ili ajibu tuhuma za makosa ambayo yanamkabili ,Sheria tunataka ichukue mkondo wake,”alisema Kamanda Mambosasa.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )