Wednesday, February 14, 2018

Katibu wa Bunge Azungumzia Afya ya Spika Job Ndugai

Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema hali ya afya ya Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyepo nchini India inaendelea vizuri.

Kagaigai amesema leo Februari 14,2018 kuwa Spika Ndugai yupo India kwa ajili ya kuangalia afya yake (check-up) na anatarajiwa kurejea nchini wakati wowote.

Katibu huyo wa Bunge amesema, “Tulikwisha kusema kwamba Spika yuko India kwa ajili ya ‘check-up’ na hali yake inaendelea vizuri.”

Alipoulizwa kuwa Spika atakuwa ughaibuni hadi lini, Kagaigai amesema: “Hilo ni kati ya daktari wake na yeye lakini ninachoweza kusema wakati wowote anaweza kurudi nchini.”

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )