Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, February 17, 2018

Mabalozi Walioapishwa Jana (Dr Salaa na Muhidin Ally) Wamuaga Makamu Wa Rais Leo

adv1
Balozi wa Tanzania nchini Nigeria  Mhe. Muhidin Ally Mboweto pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Wilbrod Peter Slaa leo wamekutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oysterbay, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga tayari kwenda kwenye vituo vyao vipya vya kazi.

Mabalozi hao waliapishwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  Ikulu jijini Dar Es Salaam .

Makamu wa Rais aliwatakia safari njema huko waendapo kwenye vituo vipya vya kazi ambapo aliwasihi kwenda kufanya kazi kwa moyo mmoja na kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais

“Hakikisheni mnaitangaza nchi yetu vizuri na kuwashawishi wawekezaji  ili waweze kuja kwa wingi, nchi yetu ina fursa za kutosha” alisema Makamu wa Rais.

Kwa upande wao Mabalozi hao walimuahidi Makamu wa Rais  kuiwakilisha nchi vizuri na kufanya kazi kizalendo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )