Loading...

Wednesday, February 7, 2018

Mbunge Chadema ahoji utekelezwaji sera ya matibabu bure kwa wazee

Mbunge Viti Maalum Jimbo la Morogoro (Chadema), Devotha Minja ameihoji serikali juu ya utekelezwaji wa sera ya huduma ya matibabu bure kwa wazee.

Minja ameyahoji hayo katika kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao cha sita cha Bunge la kumi linaloendelea mjini Dodoma, ambapo amesema wazee katika kambi ya Fungafunga iliyoko mjini Morogoro wanakosa dawa na kulazimika kununua dawa muhimu kwenye maduka ya dawa ya nje, kutokana na uhaba wa dawa uliopo kwenye Hospitali ya mkoa wa Morogoro.

“Kambi ya Fungafunga iliyoko mjini Morogoro inayohudumia wazee wengi hivi sasa wanakosa huduma ya matibabu kutokana na hospitali ya mkoa wa Morogoro kukosa dawa za kutosha, wazee wanapewa panado na dawa nyingine wanaambiwa wakanunue kwenye famasi za nje, nataka kujua sera hii ya matibabu bure kwa wazee inatekelezeka?,” amehoji.

Akijibu swali la Minja, Naibu Waziri wa Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amesema serikali inatekeleza sera hiyo kikamilifu, pia kwa sasa hakuna uhaba wa dawa kwenye hospitali za umma, kutokana na kuongezeka kwa bajeti ya dawa kutoka bilioni 30 hadi kufikia takribani bilioni 270.

“Serikali kwa mujibu wa Sera ya Afya ya mwaka 2007 imetamka wazi kwamba matibabu kwa wazee wasiojiweza yatakuwa buree na hilo tunalitekeleza kikamilifu lakini sambamba na hilo, hatuna uhaba wa dawa sasa hivi, bajeti ya dawa imeongezekasana kutoka bilioni 30 hadi  kufikia takribani bilioni 270 dawa zote muhimu zinapatikana, kama kuna suala mahsusi kuhusiana na kambi hii, devotha minja ningependa kupata maelezo ya ziada ili tushughulikie tatizo hilo,” amesema.

Aidha, Dkt. Ndugulile amesema kwa sasa serikali iko kwenye mapitio mapya ya sera, baada ya sera yam waka 2003 kupitwa na wakati, ili ihuishe mahitaji ya wazee ya sasa kwa ajili ya kutunga sheria mpya.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )