Loading...

Monday, February 5, 2018

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Aapishwa Rasmi Bungeni

Naibu Spika wa Bunge, Dkt.  Tulia Ackson amemwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dkt. Adelardus Kilangi bungeni na kumkabidhi vitendea kazi kabla ya kuanza kwa Kikao cha Tano cha Mkutano wa 11 wa Bunge, Mjini Dodoma, leo Feb 5, 2018.
 
Dkt. Kilangi ambaye amekula kiapo cha uaminifu, aliteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Mgufuli,  Februari Mosi, 2018 na Paul Ngwembe aliteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika hatua nyingine,Magufuli alimtea aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na naibu wake, Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambao waliapishwa juzi Jumamosi, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )