Loading...

Thursday, February 1, 2018

Rais Magufuli: "Sitalalamika tena,najua nitakavyofanya"

Rais John Magufuli amewapa pole Majaji kwa changamoto wanazokumbana nazo pindi wanapo shughulikia mashitaka yanayopelekwa na serikali na kuahidi kulifanyia kazi jambo hilo kabla ya mwezi Februari kuisha kwa madai ameshajifunza vya kutosha.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati alipohudhuria kilele cha maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria na uzinduzi wa mwaka mpya wa kimahakama yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo yeye binafsi ndio alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hizo akiongozana na viongozi wengine wa serikali.

"Kwa kuadhimisha siku hii ya sheria maana yake ni kwamba nchi yetu inatambua umuhimu wa sheria katika kusimamia haki, kudumisha amani na kuleta maendeleo ya nchi. Maadhimisho haya ya siku ya sheria ni muhimu kwa vile yanatoa fursa kwa vyombo vinavyohusika na masuala ya sheria na utoaji haki", alisema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli alisema bado kuna tatizo kubwa katika ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) na AG (Mwanasheria Mkuu), na ndio maana muda mwingine inawapelekea kuwapa changamoto kubwa Majaji.

"Najua mnapata shida sana mnapo-dili na mashitaka yanayoletwa na serikali mnauona kabisa ushahidi upo lakini watetezi hawajitokezi hadharani kuutetea. Mwaka jana nililalamika lakini mwaka huu nitalishughulikia vizuri. Sitalalamika tena ninajua nitakavyofanya kwa sababu nimeshajifunza vya kutosha na nimejua wapi kuna 'weakness' na wala huu mwezi wa Februari hautoisha", alisisitiza Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amewataka viongozi wengine wanaosimamia vyombo vya sheria kufuata mfano mzuri aliyouanzisha Profesa Ibrahimu Juma kwa kutowafumbia macho wahalifu wa aina yeyote ile.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )