Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, February 11, 2018

SORRY MADAM -Sehemu ya 88 & 89 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

   Phidaya akageuka nyuma na kuwaona askari wawili walio valia suti wakimfwata kwa kasi kitendo kilicho mfanya kuzidi kukimbia kwa uwezo wake wote. Rahab akiwa kwa mbali akamuona Phidaya akikatiza kwa kasi, mara hajakaa sawa akawaona askari wawili wakimfwata kwa kasi wakitoka katika majengo wakielekea kwenye maegesho ya magari. Rahab akafwata kwa nyuma ili kuwazuia askari hao, huku naye akiwa katika mwendo kasi.

Phidaya katika kutizama tizama kwake kwenye maegesho ya magari, akaona gari moja likisimama kwenye maegesho ya hapo hospitalini. Kwa haraka pasipo hata kuuliza Phidaya akafungua mlango wa nyuma wa gari hilo na kuingia na kumfanya muendeshaji aliyopo humo ndani kugeuka kwa kasi na kumuangalia.
“WEWE NI NANI?”  
Muendeshaji ambaye ni mwanamke mwenzake, alimuuliza kwa sauti ya ukali huku akiwasha taa ya ndani ya gari lake kuiona sura ya Phidaya vizuri.

ENDELEA
   Macho ya Agnes yakabaki yakimshangaa mwanamke huyo ambaye leo ndio mara yake ya kwanza kumuona. Kabla hajazumgumza kitu Agnes akashuhudia wanaume wawili mbele ya gari lake wakipokea kipigo kwa msichana ambaye anamfahamu fika. Wanaume hao wanao onekana kuwa ni walinzi wa kiongozi wa nchi, walijikuta makonde yao hayafui dafu mbele ya makonde ya Rahab anaye shusha kipigo kikali juu yao.

“Rahab”
Agnes alizungumza huku akiwasha taa za mbele za gari yake kushuhudia jinsi kifinyo hicho kinavyo tembea kwa wanaume hao. Ndani ya dakika tano wanaume hao wakawa wamevunjwa vujnwa viongo na Rahab aliye simama kwa kijiamini mbele ya gari la Agnes. Kwa haraka Agnes akashuka kwenye gari hukku akiwa na tabasamu usoni mwake.
“Rahab”
Agnes aliita huku akianza kumfwata Rahab sehemu aliyo simama, kabla hajamfikia walinzi wengine watatu wenye mitutu ya bunduki wakanza kuzifnyatua risasi zao sehemu alipo simama Rahab, ambaye hakuwa mzembe kwa kiasi hicho kwani hata kabla risasi hizo hazijamfikia akaanza kuruka sarakasi kuelekea naapo tokea Agnes ambaye kwa haraka akarudi kwenye gari na kujitosa kama alivyo ingia Phidaya.

Kwa haraka Rahab akaingia kwenye gari la Agnes.
“Go go goo”(Nenda ndenda nendaaa)
Rahab alizungumza kwa sauti ya juu na kumfanya Agnes kuwasha gari lake kwa haraka, akalirudisha nyuma kwa mwnedo wa kasi, akakata kona moja kali, alipo hakikisha amelilenga geti la kutokea, hakufanya kosa zaidi ya kukanyaga mafuta na kuondoka eneo la hospitali na kuwaacha walinzi hao wakifyatua fyatua risasi pasipo mafanikio yoyote. Mlinzi mmoja akarudi sehemu walipo acha magari yao akaingia kwenye gari moja na kuliendesha kwa kasi hadi sehemu walipo simama wezake, wakaingia ndnai ya gari na kuanza kuwafukuzia Phidaya na wezake.
                                                                                                                  ***
 Milio ya risasi inayo endelea nje ikawafanya watu kadhaa ndani ya hospitali waliyo isikia kuchanganyikiwa, mtu aliye toka katika chumba cha wagonjwa mahututi, akamfanya Shamsa kumtazama kwa muda, huku akiwa amemkazia macho.
“Huyu si Manka aliye mchukua Eddy”
Shamsa alizungumza huku akianza kupiga hatua za haraka kuelekea katika mlango alio simama Manka pamoja na walinzi wa wawili wa mzee Godwin.
“Huruhusiwi kuingia hapa binyti”

Mlinzi mmoja alizungumza huku akimzuia Shamsa kwa mkono, Manka akamta jicho la dharua Shamsa, kisha akaendeleak usikilizia milio hiyo ya bunduki ni wapi inapo tokea. Kwa kasi ya ajabu Shamsa mguu wake mmoja akaukanyaga kwenye paja la mlinzi huyo, akajirusha kwajuu na kumkalia mabegani, bila hata ya huruma akamvuja shingo na kuanguka naye chini na kumfanya Manka na mlinzi aliye baki kubaki wameduwaa. Mlinzi akataka kuchomoa bastola yake, ila tayari amesha chelewa kwani Shamsa alisha mfikia na kumpiga mtama ulio muangusha chini, hata kabla hajajinyanyua tayari shingo yake ilisha vunjwa.
Shamsa akanyanyuka huku akimkazia macho Manka aliye anza kurudi nyuma na kuingia chumbani huku Shamsa akimfwata kwa mbele.

Shamsa alipo muona Eddy akiwa amelala kwenye kitanda akabaki ameduwaa kwa sekunde kadhaa, jambo lililo kuwa ni kosa kubwa sana kwake kwa maana Manka, alimshushia teka zito la tumbo lililo muangusha chini. Maumivu ya tumbo aliyo yapata Shamsa yakamfanya ajinyanyua chini taratibu huku akimtazama Manka aliye jiweka tayari kwa mashambulizi.
Sa Yoo na madam Merry wakakutana kwneye kordo inayo elekea kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi. Wakashuhudia walinzi wawili wakiwa wamelala chini ya sakafu nje ya chumba kimoja. Kwa haraka wakaanza kukimbia hadi kwenye mlango wa chumba hicho na kumshuhudia Shamsa anavyo pokea kichapo kutoka kwa Manka. Wote wawili wakaingia ndani na kuanza kumshambulia Manka, kila mmoja aliweza kumshambulia jinsi alivyo weza, aliye rusha kofi sawa, aliye vua kiatu na kumtandika sawa, ilimradi walihitaji kumuokoa Eddy aliye muona amelala kitandani.

“Mchukueni Eddy muondoke naye mimi ninamshuhulikia huyu”
Shamsa alizungumza huku akinyanyuka, Madam Merya na Sa Yoo hawakupoteza muda baada ya kumuona Manka amelala chini akiwa yupo hoi taabani. Kutokana kitanda alicho lalia Eddy kina matairi, walicho kifanya ni kuchomoa waya wa umeme wa mashinye ya kuhesabu mapigo ya moyo iliyopo pembeni ya kitanda hicho, na kuanza kukisukuma kutoka nje.
“Tupite njia hii”
Madam Mery alizungumza, Sa Yoo akatii wakaanza kukisukuma kitanda hicho hadi nje kwenye maegesho ya magari cha kushukuru Mungu hapakuwa na mtu hata mmoja, kutokana milio ya risasi hiyo ilisikika katika eneo hilo na raisi wote walikimbia japo ni usiku.

“Kwenye gari hili hawezi kuingia”
“Itakuwaje sasa?”
Sa Yoo akaitazama gari la wagonjwa lililopo kwenye maegesho hayo kwa haraka akalikimbilia, akajaribu kufungua mlango wa upende wa dereva kwa habati nzuri akaukuta upo wazi, kwnai ni muda mchache gari hilo limeleta mgonjwa hapo hospitalini, kingine cha kumshukuru Mungu hata dereva aliweza kusahau fungua kwneye mskani wa gari hilo. Kwa haraka Sa Yoo akaingia na kuliwasha gari hilo akalirudisha taratibu hadi sehemu kilipo kitanda, akshuka kwa haraka, akazunguka nyuma wakasaidiana na Madan Mery kumuingia Eddya kaiwa na kitanda chake kisha madam Mery akaingia nyuma na kufunga mlango na Sa Yoo akarudi mbele, akakanyaga mafuta na kuondoka eneo hilop la hospitali.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )