Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, February 12, 2018

SORRY MADAM -Sehemu ya 90 & 91 (Destination of my enemies)


MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA  

“Na tambua Eddy nimesha mfahamu, na Eddy huyo huyo ndio atakaye kuja kuja kukuangamiza, na kuanzia hivi sasa usinihusishe na mipango yako ya kikatili”
Manka alizungumza kwa hasira huku akijikongoja kutoka mlangoni ila kabla hajafika mlangoni huku nyuma akasikia bastola  ikikokiwa, taratibu akageuka na kumkuta Mzee Godwin akiwa amemnyooshea bastola ya uso, huku macho yam zee Godwin yakiwa yametawaliwa na ukungu mwekundu wa hasira hadi mkono wake ulio shika bastola ukawa unatetemeka.

ENDELEA
“Na mimi unahitaji kuniua, kama unavyo hitaji kumuua Eddy?”
Manka alizungumza huku machozi yakimwagika, Mzee Godwin akaendelea kumshikilia Manka bastola huku akizidi kutetemeka kwa hasira.
“Kwa nini hukumuua Mery nilipo kuagiza pale Arusha?”
“Damu ni nzito kuliko maji baba, na Mungu aliweza kunipa roho ya ujasiri ya kumuacha akiwa hai, kumbe ni mama yangu mdogo. Nimekua bila ya kuwa na mama, ila wewe hulioni hilo hadi unahitaji nimuue mama yangu mdogo si ndio?”

Hasira ya Manka na kulia kwake kukamfanya aishiwe nguvu, za miguu na kujikuta akianguka chini. Kwa haraka mzee Godwin akairudisha bastola yake mkononi na kumnyanyua Manka na kumuweka kitandani kisha akatoka chumbani humo akiwa na hasira kali.
“Hakikisheni Manka hatoki humu ndani”
“Sawa mkuu”
Mzee Godwin akaondoka huku akiwa na mlinzi wake anaye muamini, moja kwa moja wakarudi ikulu kuendelea na majukumu yao.
                                                                                                               ***
Rahab, Phidaya na Agnes walikesha wakipiga hadithi mbalimbali, kila mmoja akijaribu kusimulia maisha yake ya utotoni na usichana.. Hadi inafika alfajiri hapakuwa na aliye pata hata lepe la usingizi, kila mmoja wao aliweza kufikiria mambo yanayo muhusu kwenye maisha yake hususani kwa wakati huu.
“Yaani Erickson ninampenda sana, na endapo nitakuja kujua ana mwanamke mwengine nitahakikisha nina muua huyo mwanake”
Agnes alizungumza kwa kujiamini na kuwafanya Phidaya na Rahab kutazama, kabla ya Phidaya ajazungumza kitu Rahab akamuwahi.

“Shoga wewe nawe kwa wivu, unamuua mwanamke mwenzako kisa mwanaume?”
“Ahaaa weee Erickson wangu mtamu sana, yaani ni mwanaume shababi, anaye jua kucheza na mwanake sita kwa sita”
“Cha kufanya inabidi ikitimu saa mbili uende ukamuangalie hospitalini”
“Hapo Rahab umezungumza poit huwa ninakupendea hapo tu”
“Ndio hivyo usijikalie hapa kumbe kama ulivyo tuambia mpenzi wako ni mgonjwa”
“Sawa”
Muda wote huo Phidaya alikaa kimya akiyafikiria maneno ya Agnes jinsi yalivyo utibua moyo wake, hata urafiki ambao ulikuwa kwa masaa machache tayari umesha ingia shubiri. Wakaandaa kifungua kinywa, kila mtu akanywa kwa jinsi alivyo weza kunywa chai hiyo yenye itafunwa vingi.

Phidaya akarudi sebleni alipo iacha bahasha yake, akaichukua pamoja na karatasi iliyopo pembeni ambayo hakuiweka kwenye bahasha hiyo. Kabla hajaiingiza karatasi hiyo ndani ya bahasha akaipitishia macho taratibu ili kufahamu ni karatasi za nini. Phidaya hakuamini kitu alicho kiona kimeandikwa kwenye karatasi hiyo, maelezo yanaonyesha uhusiano alio kuwa nao Erickson ambaye ni Eddy pamoja na Manka ambaye ni wifi yake.

‘Imekuwaje hadi ukweli umejulikana?’
Phidaya alijiuliza huku akiketi kwenye sofa, macho yake yakawa na kazi ya kuirudia rudia karatasi hiyo mara kadha.
‘Ila dokta aliye fanya hivi alisha kufa’
Phidaya alizidi kuzungumza mwenyewe huku akiitazama karatasi hiyo, hadi Rahab anafika sebleni hapo, ndipo alipo iingiza karatasi hiyo kwenye bahasha.
“Karatasi za nini?”
Rahab aliuliza huku akijirusha kwenye sofa. Phidaya hakujibu kity chochote zaidi ya kukaa kimya.
“Vipi mbona kimya?”
“Agnes yupo wapi?”
“Nimemuacha akielekea chumbani kwake kuoga”
“Kuna kitu nahisi hakipo sawa”
“Ahaaa kama ni mada hizo tutazizungumza tukiondoka hapa”
Rahab alizunguzma kwa sauti ya chini huku akimtazama Phidaya kwa macho makali. Haukupita muda sana Agnes akatoka akiwa amevalia suti nyeusi. Akamrushia Rahab funguo ya gari moja huku yeye akiwa na funguo ya gari la serikali.
“Mutatumia gari hiyo”

“Una magari mangapi shosti?”
“Mmmm huko uwani yamejazana mengi, sikumbuki kwa haraka nina magari mangapi, si unajua kwamba starehe yangu kubwa ni magari”
“Wewe kiboko”
Wakatoka kwa pamoja na kuelekea eneo la nyuma la nyumba ya Agnes ambapo kuna banda kubwa alilo lijenga lenye magari mengi yaliyo funikwa. Rahab akayahesabu kwa haraka haraka akapata idadi ya magari ishirini na tano.
”Wee mtoto wa kike magari yote haya ni ya nini?”
“Wee acha tu sina mtoto sina ndugu, pesa yangu yote ninayo ipata ni kununua magari. Hapo kuna magari ambayo tangu niyanunue, nimeyaendesha kutoka bandarini hadi hapa”
“Wee kiboko sasa hii funguo uliyo nipa nitafungulia gari lipi?”
“Minya rimoti, litakalo piga alamu ndio hilo hilo”
Rahab akafanya kama alivyo ambia, gari la pembeni lake likaanza kupiga alamu, wakalifunua turubai lililo lifunika gari hilo.

“Hiyo ni Alteza new modern zimetoka mwaka huu”
Agnes alizungumza huku akilitazama gari yake hiyo mpya kabisa. Rahab akaingia na kuliwasha gari hilo.
‘Mamaeee huyu msenge ana hela’
Rahab alijisemea kimoyo moyo, baada ya gari hiyo kumuonyesha tanki lake limejaa mafuta.  Rahab akafungua kioo cha upande wake ili kuzungumza na Agnes.
“Wee mtoto sikuwezi”
“Kwa nini?”
“Gari ipo full tank, nilidhani itakuwa na mafuta ya kulisukumia hadi sheli”
“Nyoo, gari zote hapa unapo ziona zipo full tank. Sasa utawasiliana na mimi ukiwa na simu, au hadi simu nikupe”
“Acha ujinga, nitanunua”
“Haya mwaya, Phidaya karibuni tena jamani”
“Asante”

Phidaya akaingia ndani ya gari, wakaondoka na kumuacha Agnes akiingia kwenye gari lake lenye namba za usajili za wizara yake. Moja kwa moja Agnes akaanzia hospitali ya Agakhan, ambapo akaelekea kwa daktari mkuu wa hospitali hiyo. Akamuuliza kuhusiana na mgonjwa wake ambaye ni Erickson Ford, majibu aliyo kutana nayo yakamshosha sana.
“Ameibiwaje ibibiwaje?”
“Kusmea kweli mimi jana sikuwepo usiku, ila nasikia hata walinzi wa raisi walishindwa kuwazuia hao walio muiba”
“Mungu wangu sasa itakuwaje?”
“Ndio hapo naona muheshimiwa ana lishuhulikia huli, naamini atapatikana tu”
“Sawa nashukuru dokta”
Agnes akaondoka hospitalini hapo huku akiwa amejawa na mawazo chungu nzima, hakujua ni nini anacho weza kukifanya ili kumpata Erickson wake.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )