Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 14, 2018

SORRY MADAM -Sehemu ya 92 & 93 (Destination of my enemies)

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Sa Yoo akajikuta akishangilia kwa furaha, ila sura ya Madam Mery ikapoteza furaha, na kumfanya Eddy naye kupoteza furaha yake.
“Ina maana hamuniamini au?”  
“Phidaya nina mjua Godwin hawezi kukamatika kiholela kiasi hicho”
Madam Mery alizungumza kwa msisitizo, huku akiwa amemkazia macho madam Mery
“Jamani nimemkuta akiwa amelala chini mguuni amepigwa risasi”
“Kwa nini tubishane twendeni tukamuone”
Sa Yoo akaanza kukisukuma kitanda cha Eddy huku Phidaya na Madam Mery wakiwa wametangulia mbele, huku Shamsa akifwata kwa nyuma. Wakatoka kwenye vyumba hivyo na kwenda nje. Walipo fika kila mmoja akabaki ameduwaa hususani Phidaya kwa maana Raisi Godwin na Rahab wametoweka eneo hilo

ENDELEA
“Wamekwenda wapi?”
Phidaya aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka. Madma Mery akajikuta akikaa chini, huku nguvu za mwili zikiwa zimemuishia.
“Tuondokeni eneo hili si salama”
Eddy alizungumza huku akijaribu kukaa kwenye kitanda, maumivu makali aliyo yapata kwenye mbavu zake hayakumzuia kabisa kuweza kunyanyuka na kukaa kitako.
“Utataka kwenda wapi Eddy?”
“Ni bora nyinyi kuondoka kuliko kuingia mikononi mwa askari”

“Unataka kusema kwamba…….”
Phidaya aliuliza huku macho yake akiwa amemtolea Eddy aliye lala kwenye kitanda hicho.
“Ondokeni eneo hili sio salamaa”
Eddy alizungumza kwa msisitizo na kuwafanya  Shamsa kuelewa maana yake ni nini. Shamsa kwa haraka akaingia ndani, moja kwa moja akaelekea katika chumba ambacho walikuwepo. Akachukua mbastola nne zenye magazine zilizo jaa risasi kisha akatoka nje kwa haraka.
“Inabidi kuondoka eneo hili sasa hivi”
“Na Eddy?”
“Mimi mutaniacha hapa, ondokeni”
Taarifa hiyo, ikauingiza moyo wa Phidaya simanzi kubwa sana, kwa maana hakujua ni kwanini mume wake amechukua maamuzi kama hayo. Kwa haraka akamfwata Eddy kitandani na kukumbatiana huku Phidaya machozi yakimwagika, na Eddy machozi yakimlenga lenga.

“Nitakuwa salama”
Phidaya hakujibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuzidi kumwagikwa na machozi, tayari Shamsa alisha ingia kwenye moja ya gari, ambalo ni mali ya ikulu. Madam Mery na Sa Yoo nao wote wakaingia ndani ya gari hilo na kumsubiria Phidaya anaye endelea kumng’ang’ania mume wake.
“Nenda mke wangu nitakuwa salama”
“Niahidi hauto kufa?”
“Nakuahidi, kimbia kabla askari hawajafika hapa”
Phidaya akamuachia Eddy na kumpiga busu la mdomo, kisha akashuka kwenye ngazi hizo kwa haraka na kuingia ndani ya gari, Shamsa ambaye tayari alisha lifungua geti hilo muda alipo kuwa anashuka chini, akakanyaga mafuta ya gari hilo ambalo ni aina ya Aud 5q lenye sifa ya kuto kuingia risasi na ndio gari ambalo hutembelea raisi Godwin.
Kipindi gari hiyo inamalizikia kutoka nje, machozi yakatiririka usoni mwa Eddy ambaye hakuweza kujumuika katika safari hiyo, kwanza kutokana na mshono wa oparesheni aliyo fanyiwa jana tu, pili ni kutokana hajulikani kama yeye ndio Eddy, ila anajulikana kwa jina la Erickson Forrd hii ni kutokana na sura yake.

Hazikupita hata dakika tano, ving’ora vya gari za polisi pamoja na usalama wa taifa vikasikika nje ya nyumba ya Eddy. Alicho kifanya Eddy ni kujilaza kitandani hapo huku machozi yakiendelea kumwagika.
Askari wengi wenye bunduki mikononi mwao wakaingia ndani humo kwa umakini, wakaanza kukagua maiti moja baada ya nyingine.
“Erickson”
Eddy akamuona Manka akimfwata sehemu alipo lala. Taratibu Manka akapiga magoti chini, na kumbusu Eddy mdomoni.
“Nashukuru Mungu nimekupata”
Eddy hakujibu kitu zaidi ya kumwagikwa na machozi usoni mwake. Madaktari wa jeshi walio fika eneo hilo la tukio, wakamchukua Eddy na kumuingiza kwenye gari ya wagonjwa, huku akiambatana na Manka ambaye hakuhitaji kumpoteza tena.

Askari walio baki huku nyuma kazi yao ikwa ni miili ya askari walio pigwa risasi, kati ya askari ishirini walio fika katika eneo hilo, ni mmoja tu ambaye ni mlinzi wa raisi Godwin aliye weza kuwa hai japo hali yake ni mbaya
“Muheshimiwa raisi…..a…me..ch…..u”
Hakumalizia kitu alicho kuwa anakizungumza akapoteza fahamu.
“Muwahisheni hospitalini, huyu atatufaa”
Mkuu wa kitengo cha polisi kanda maalimu bwana Erinest Komba aliwaeleza vijana wake, ambao wakafwata amri kama alivyo zungumza mkuu wao. Habari ya raisi Godwin kutoweka ikaanza kusambaa kwa kasi kupitia mitandao  ya kijamii, huku vituo vya televishion na maredio vikiwa vinatafuta ukweli juu ya jambo hilo. Hapakuwa na mkuu yoyote wa jeshi aliye weza kudhibitihs habari hizo kwa maana hapakuwa na mtu mwenye ushahidi katika hilo.
                                                                                                         ***
“Jikaze usilie, unavyo lia unadhani mimi nitafanyaje?”
Shamsa alizungumza huku akimtazama Phidaya anaye lia njia mzima
“Ila mume wangu atakuwa kwenye matatizo”
“Sio rahisi kwa Eddy kuingia kwenye matatizo ndio maana akatuambia tuondoke”
Muda wote madam Mery akawa kimya akilichunguza gari hilo, kwa bahati nzuri akaona kifaa maalumu ambacho kipo siti ya nyuma ya dereva eneo alilo kaa yeye kinacho weza kuonyesha ni sehemu gani raisi yupo, hata walinzi wake wanapo kaa ikulu.
“Shamsa simamisha gari?”
“Kuna nini?”
“Simamisha gari kwanza”
Shamsa ikambidi kutii kile kitu ambacho madam Mery amemueleza, kwa haraka madam Mery akashaka kwenye gari, akamuomba Shamsa kufungua buti ya gari, Shamsa akaminya batani iliyo ruhusu buti ya gari hilo kufunguka, madam Mery akalinyanyua, akakuta kifaa kidogo kinacho ongoza kifaa alicho kiona ndani ya gari hilo.

“Ohoo ni GPRs system”
Sa Yoo alizungumza mara baada ya kuona kifaa hicho.
“Ndio nini?”
Shamsa aliuliza mara baada ya kushuka kwenye gari na kuzunguka nyuma kwenye buti ya gari hilo.
“Sehemu yoyote  tunapo kwenda nah ii gari lazima tuonekane”
“Sasa inakuwaje?”
Hata kabla Sa Yoo hajajibu swali hilo, wakaziona gari nne nyeusi, aina ya GVC zinazo piga ving’ora zikiwafwata kwa kasi katika eneo hilo.
“Ohooo rudini kwenye gari wote”
Shamsa alizungumza kwa haraka akafunga buti ya gari hilo, wote wakaingia ndani gari, bila ya kupoteza muda, Shamsa akakanyaga mafuta ya gari na kuondoka eneo hilo kwa kasi kubwa.
“Fungeni mikanda”
Shamsa alizungumza huku akifunga mkanda wa siti aliyo kalia. Gari  hizo nne za makachero wa usalama wa taifa, zikazidi kuifukuza gari hiyo ya raisi huku mkuu wao aliye panda gari la mbele akiwa na simu maalumu inayo onyesha gari hilo la raisi kila sehemu anapo kwenda.

“Ongeza mwendo, hawa watu ndio walio mteka raisi”
“Sawa mkuu”
Dereva huyo, ambaye naye ni kachero anaye sifika katika maswala ya uendeshaji wa gari kwa kasi, akawa ndio kama amechochewa, akazidi kukanyaga mafuta kwa kasi, hadi madereva wezake wanao endesha magri matatu yaliyo nyuma yao akawaacha kwa umbali kidogo.
“Wanazidi kutufwata”
Sa Yoo alizungumza huku mara kwa mara akigeuza kichwa chake nyuma. Katika uendeshaji wa gari, Shamsa anajimudu sana, ila kitu kinacho mfelisha kwa wakati huu, ni bega lake lililo pigwa risasi, na ndio kwanza kidonda hakijapona na maumivu anayo yaoata hapo ni makali kupindukia sema tu anajikaza kuwaokoa wezake kwa maana wakiingia mikononi mwa Makachero hao, hakuna mtu mwenye jawabu la kujua ni nini atakacho fanywa.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )