Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, February 16, 2018

SORRY MADAM -Sehemu ya 94 & 95 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

“Nifwateni mimi”
Binti huyo wa kimasai alizungumza na kushuka kwenye kichuguu hicho. Wote wakamfwata kwa nyuma akwapeleka kwenye moja ya handaki wanalo jificha pale kunapo tokea uvamizi.  Wakakuta wamama na watoto pamoja na wazee wakiwa wamasha ingia kwenye handaki hilo wamejificha baada ya kupigwa kwa vigelegele hivyo.
“Munaweza kujificha humu na maadui wasijue ni wapi nyinyi mulipo”
Hata kabla hawajazungumza chochote, milio ya risasi ikaanza kusikika ikirindima nje ikiashiria kwamba watu hao walio kuja kwenye kijiji hicho si wema kabisa.

ENDELEA
 Karibia watu wote ndani ya handaki miili yao ilipatwa na woga. Wamama walio kuwa na watoto wadogo waliwakumbatia watoto wao huku wakiachia vilio vilivyo wafanya Sa Yoo na Shamsa kushangaa.
“Hatuwezi kukaa humu ndani na kuona watu wasio wenye hatia wakiwa wanakufa pasipo sababu ya msingi”
Phidaya alizungumza huku akiwatazama Shamsa na Sa Yoo ambao muda mwingi waliwatazama wanamama hao na watoto wanavyo angua vilio.
“Una maana gani?”
Binti huyoo wa kimasai aliuliza huku mwili ukimtetemaka. Shamsa akataka kuchomoa bastola yake, ila Sa Yoo akamuwahi mkono huo na kumzuia.
“Sio sehemu yake hii”
Sa Yoo alizungumza huku akiondoka kwenye handaki hili, akapandisha ngazi huku nyuma yake akifwatia Phidaya na Shamsa.

“Tafadhali usitoke baki humu ndani”
Shamsa alimueleza binti wa kimasai ambaye aliwafwata kwa nyuma walipo kuwa wakitaka kutoka. Bimti huyo akawa muelewa na kurudi ndani ya handaki.
   Milio ya risasi iliendelea kurindima, huku vijana wa kimasai wanao tumia silaha za jadi wakiendelea kuteketea kwa maana uweozo wao wa kupambana ni mdogo kuliko uwezo wa wanajeshi hao.
Hapakuwa na mazungumzo zaidi ya kuhakikisha kwamba wanatetea kijiji hicho kinacho poteza watu wake kwa sababu yao. Kila mmoja akakimbilia katika sehemu  ambayo anaweza kuhakikisha kwamba haonekani na kuanza kujibu mashambulizi ya wanajeshi hao
                                                                                                                      ***
“ARGAAAAAAAAAAAAAAAAAAA…………..”
Ukelele mkali ulisikia katika moja ya chumba kilichopo chini ya ardhi kwenye handaki ambalo, mikaka kadhaa ya nyuma iliyo pita, lilikuwa likitumika kama maficho ya majambazi wa kike walio tokea kuitingisha serikali ya Tanzania.
Sura ya Rahab iliyo jaa hasira na uchungu mwingi ikaendelea kuonekana mbele ya uso wa raisi Godwin ambaye amening’inizwa hewani kwa mikono yake kufungwa na kamba ngumu ya manila, kila mkono umefungwa upande wake, na miguu yake nayo imefungwa kila mmoja upande wake. Huku mwili wake ukiwa hauna nguo hata moja.
Kitu ambacho Rahab anakifanya ni kila mara kupiga teke kwa chini kwenye sehemu za siri za Mzee Godwin na kumfanya atoe ukelele mkali.
“Niue tu lakini sio kunifanyia unyama wa aina hii”
Mzee Godwin aliye jaa damu kwneye sura yake iliyo chakaa kwa kipigo kilali alicho patiwa na Rahab, alizungumza huku akimtazama Rahab, aliye mjibu kwa kumtandika ngumi moja kali ya uso, na kuzifanya damu kuzidi kumtoka raisi Godwin kwenye sura yake.

“Mume wangu Praygod, alikufa kifo kikali cha kikatili na wewe ndio msababishaji wa hili”
“Mimi sifahamu hilo”
“Ahaaa ufahamu si ndio?”
“Ndio sifahamu”
“Basi kwa kipigo hichi utafahamu tu”
Rahab akachukua mashine maalumu ya shoti, akachukua nyaya mbili za hasi na chanya moja akaifunga katika uume wa mzee Godwin na mwengine akaufunga kwenye gololi za mzee huyo, kisha akarudi mezani ilipo mashine hiyo yenye swichi ya kuongezea mtetemesho wa shoti.

Bila hata ya huruma, Rahab akaiwasha mashine hiyo na kumfanya mzee Godwin kutetemeshwa karibia mwili mzima. Mzee Godwin alizidi kulia kwa maumivu makali sana anayo yapata. Tangu kwenye maisha yake yote hakuwahi kuweza kukutana na maumivu makali ya namna hiyo japo alikuwa ni mwanajeshi na aliweza kukutana na waalifu wengi alio weza kuwabana na mashine hiyo ya shoti ila kwa sehemu alipo wekewa nyanya hio ndivyo jinsi alivyo zidi kuona maisha yake yanakwenda ukingoni hata kabla ya kufanikisha malengo yake ya kuifanya nchi ya Tanzania kuwa na utawala wa kifalme na si wa uraisi tena.

Maumivu makali aliyo yapata yakapelekea mzee Godwin kupoteza fahamu hapo hapo. Hilo wala halikumuogopesha Rahab alicho kifanya ni kuzima mashine hiyo. Akachukua ndoo kubwa, akaingia bafuni akakinga maji kwenye bomba hadi, ndoo hiyo ikajaa. Akarudi nayo kwenye chumba cha mateso, akamwagia maji hayo mzee Godwin na kumfanya kustuka kutoka katika hali ya kupoteza fahamu.
“Zoezi letu linaendelea pale pale”

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )