Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, February 8, 2018

Wahamiaji Walowezi Watakiwa Kujiorodhesha Uhamiaji

IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imewataka  wahamiaji walowezi kujiorodheshwa katika ofisi zao za uhamiaji  wilaya.

Lengo ni kwamba baada ya kufanya hivyo watapewa vibali vya ukaazi vitavyowafanya kuishi nchini kwa mujibu wa sheria , kanuni na taratibu.

Hayo yamesemwa jana  jijini Dar es Salaam,  na Naibu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Petro Malima na kuwa zoezi la  uandikishaji wahamiaji walowezi ni la nchi nzima.

“Hivyo kwa wahamiaji walowezi lazima wajiorodheshe kwa kuwa na picha tatu za Paspoti zilizo katika wakati na wenye watoto wanatakiwa kuwa na picha tatu hizo”, alisema.

Aliongeza kwa wale wataofanya hivyo watatambulika na kuendelea kuishi nchini bila kusumbuliwa kuhusu masuala ya uhamiaji na kutofautisha na wakimbizi na wahamiaji haramu.

Malima alisema wageni wote wanatakiwa kuitikia mwito huo wa Serikali pamoja na wale ambao wanaishi nchini na  kufanyakazi au biashara kinyume na sheria za nchi wanatakiwa kufika katika ofisi za wilaya ili  kuhalalisha ukaazi na kupewa vibali vinavyostahili kwa mujibu wa sheria za nchi.

Alisema  yeyote atakayejificha katika mchakato huo na baadaye kubainika anaishi kinyume cha cha sheria hatua kali zitachukuliwa.

Hatua hizo ni pamoja na kufukuzwa nchini mara moja au kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kukiuka sheria.

Aidha Malima alisema kuna matapeli wamekuwa wakiwasumbua wageni wanaoingia nchini kwa kudai wao ni askari au maofisa wa uhamiaji na wakiwa hawana hata sare.

“Viongozi wetu wanajitahidi kwa kila hali kuitangaza nchi yetu na kuvutia wawekezaji sisi uhamiaji Dar es Salaam hatuwezi kukaa kimya na kuona hii ni nia njema ya Serikali inaharibiwa na watu wachache wasiotakia mema nchi yetu."
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )