Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, February 12, 2018

Watanzania Waaswa Kuwa Wazalendo Wa Kweli Zoezi La Uandikishaji Vitambulisho Vya Taifa Unaoendelea Nchini

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dr. Mwiguli Lameck Nchemba awewataka watanzania kuwa wazalendo wa kweli kwenye Usajili wa Vitambulisho vya Taifa unaoendelea kwenye mikoa 19 ya Tanzania kwa kuwafichua wale wote wanaojipenyeza kutaka kusajiliwa kama Raia.

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizindua shughuli za Usajili na Utambuzi wa Watu katika Mkoa wa Morogoro Jumamosi katika viwanja vya Shujaa mkoani humo na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndugu Andrew Massawe akisoma taarifa ya zoezi la Usajili na Utambuzi  wa Watu kwa mikoa 19 inayoendelea na Usajili; alisema mkoa wa Morogoro unakusudiwa kusajili zaidi ya wananchi 960,000 wenye umri wa miaka 18  na kuendelea. Zoezi ambalo limepangwa kukamilika kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili,2018.

“ Mkoa wa Morogoro zoezi litahusisha Wilaya zote isipokuwa Kilombero ambayo ilikuwa Wilaya ya kwanza ya mfano kufanyiwa usajili mwaka 2012 na hivyo idadi kubwa ya wananchi wake tayari wana Vitambulisho vya Taifa na kwasasa wanaosajiliwa ni wale wanaotimiza umri wa miaka 18 na wanaohamia “ alisisitiza

Aidha ndugu Massawe amlimweleza Mhe. Waziri mbali na Usajili Mamlaka kwa kushirikiana na wadau wengine imeanza matumizi ya Vitambulisho vya Taifa ikiwemo Usajili wa Makampuni unaofanywa na Brella ambao kwa sasa unataka kila anayesajili Kampuni kuwa na Kitambulisho cha Taifa. Huduma nyingine ambazo kwa sasa huwezi kuzipata bila kuwa na Kitambulisho cha Taifa ni upatikanaji wa Hati za kusafiria(Passport), Usajili wa namba za simu na huduma nyingine za kifedha n.k

Katika hotuba yake Mhe. Waziri alikemea vikali tabia ya baadhi ya watendaji na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji kudai posho au kuhusisha michango na tozo mbalimbali wakati wa kuwasajili wananchi wakati zoezi hilo ni bure. 

Alisisitiza Mamlaka  zote za Serikali kuhakikisha zinasisimia na kutoa ushirikiano kwa NIDA kuhakikisha wananchi wote wenye sifa wanasajiliwa kwa wakati wakiwemo Wageni na Wakimbizi kwani shughuli ya usajili kwa sasa inahusisha makundi yote.  Pindi wakati utakapofika kwa wale wote ambao watakuwa hawakusajiliwa watakuwa na cha kujieleza kwanini hawakusajiliwa Vitambulisho vya Taifa wakati Serikali imewekeza fedha nyingi kukamilisha zoezi hili.

Alisisitiza Usajili Vitambulisho vya Taifa si hiyari ni wajibu wa kila Raia, Mgeni na Mkimbizi kusajiliwa kwa kufuata taratibu, sharia na kanuni za Usajili zinazosimamiwa wakati wa utekelezaji wa Usajili.

“ Kama mnavyofahamu Serikali ya Awamu ya Tano chini Mhe. Dr. John Pombe Magufuli ina vipaumbele vingi na mahitaji kwa wananchi ni mengi. Sasa Rais ameacha mambo mengine akaamua kuwekeza kwenye Vitambulisho vya Taifa mradi unaoigharimu Serikali fedha nyingi sana; sasa ole wao ambao hawatasajiliwa kwa visingizio visivyokuwa na msingi” alisisitiza

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dr. Kebwe Steven Kebwe aliwataka wananchi wa Morogoro kujitokeza kwa wingi kwenye Usajili wa Vitambulisho vya Taifa unaoendelea maeneo mbalimbali ya mkoa huo na kusisitiza hatowafumbia macho wale wote watakao husisha zoezi hilo na itikadi za vyama au dini, au kudai rushwa kuwahudumia wananchi pindi wanapojitokeza kwenye vituo vya kusajiliwa.

Zoezi la Usajili wanachi Vitambulisho vya Taifa linakusudiwa kumalizika mwezi Desemba mwaka huu kwa wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea kuwa wamesajiliwa na kupata namba za Utambulisho wa Taifa (NIN) wakati hatua za Uzalishaji zikiendelea sambamba na kuvigawa kwa wananchi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )