Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 23, 2018

Zitto Kabwe akamatwa Morogoro, Polisi watuhumu ziara yake kuwa kinyume cha sheria

adv1
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amechukuliwa maelezo katika Kituo Kituo cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro, baada ya kukamatwa  jana kwa tuhuma za kufanya mikutano kinyume na sheria.

Wakili wa Zitto Emmanuel Lazarus Mvula, amesema Polisi inatuhumu ziara ya ACT ya kutembelea madiwani wa chama hicho katika kata mbalimbali kwenye mikoa nane kwamba ni kosa kisheria.

“Ndugu Zitto ametuhumiwa kufanya Unlawful Assembly S. 74 cap 16 ya sheria ya kanuni ya adhabu, lakini kosa hilo amefunguliwa peke yake tu. Baada ya kuandika maelezo tokea saa 4:42 usiku wa jana mpaka 5:40 usiku, Jeshi la Polisi wamekataa kumpa dhamana kwa maelezo wanasubiri maelekezo kutoka juu,” amesema.

Wakili Mvula ameeleza kuwa, Zitto amewekwa mahabusu katika kituo kikuu cha polisi Morogoro.

“Polisi imekataa kusema kama dhamana ipo wazi ama la, na kama ipo wazi masharti yake ni yapi, na wamekataa kusema iwapo leo watampeleka mahakamani kwa mujibu wa sheria au la,” amesema.  
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )