Wednesday, March 7, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 27 na 28)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA  

“Halooo”  
“Halooo Dany, nimekuja wewe ni nani sasa. Na hapa ninapo zungumza nina mtu wako anaitwa Lukasi msikilizee anacho kipata”
“Ahaaa, nakufaaaaa, uuuuuuuuuu”
Nilisikia sauti ya Luka akilia kwa uchungu mkali akionekana kukupoea kipigo kikali sana kutoka kwa watu walio mkamata na sauti hii sio ngeni kabisa kwangu kwa maana ni meya niliye toka kumkoromea masaa machache nyuma.
“Rafiki yako anaelekea kufa sasa, usipo leta Nyaraka ndani ya nusu saa, baba kijacho anakwenda kuiaga dunia Paaaaaaaaaaaaaaaaaaa”
Nikasikia mlio wa risasi, kisha simu ikakatwa, na kujikuta nikitazamana na Latifa anaye mwagikwa jasho uso mzima.
                                                                                          
ENDELEA
Taratibu nikaishusha simu ya Latifa kutoka sikioni mwangu huku nikiwa na wasiwasi mwingi sana, sikujua hata imekuwaje hadi Luka akaingia mikononi mwa meya.
“Viatu hivi na soksi ukivaa utatokelezeajeee”
Sauti ya mama mkubwa ilinistua na kujikuta nikimgeukia na kumtazama huku nikiweka sura ya tabasamu feki usoni mwangu ili asifahamu ni kitu gani ambacho kinaendelea.
“Vipi mbona juu juu, mwenzako anaonekana kama hana raha?”
“Ahaa ni simu ya kibiashara kuna mzigo wake umezuiwa bandarini”
Ilinibidi kumuongopea mama mkubwa.
“Kodi nini?”
“Ndio mama”
Latifa alijibu kuliongezea uzito swala hili nililo lidanganya.
“Ahaa hembu jitaidini wangu, na huyu raisi wa sasa hataki mchezo, munaweza kujikuta munaishia pabaya na biashara zinakufa”
“Ni kweli mama”
Latifa alizungumza huku akionyesha sura ya furaha kidogo ila kusema kweli wote hapa akili zetu zimechanganyikiwa. Nikavaa soksi kisha viatu. Kwa harka anikarudi chumba cha wageni, nikachukua begi lenye nyaraka na kurudi nazo sebleni.

“Mama una photocopy mashine?”
“Ndio ipo stoo, ila ni siku nyingi haijatumia sijuia kama inafanya kazi bado”
“Naomba unionyeshe mama yangu”
Tukaongozana na mama mkubwa hadi stoo, akanionyesha mashine hiyo, nikajaribu kuiwasha haikuwaka.
“Hujachomeka waya kwenye soketi”
Ikanibidi kuchomeka waye kwenye soketi kisha nikaiwasha, kwa bahati nzuri ikawaka. Stoo hapo kuna karatasi nyeupa za kutolea photo copy. Nikaanza kazi ya kutoa nyaraka hizo photo copy kisha nikamkabidhi hizo nilizo zitoa mama mkubwa.
“Akija mama naomba umkabidhi huu mzigo”
“Sawa”
Tukatoka hapo sebleni na kuelekea sebleni, tukaaga kisha tukatoka na Latifa, moja kwa moja tukaeleka kwenye gari. Nikaliwasha gari, na kukuta mafuta yakiwa yamejaa kwenye tanki lake. Nikaliweka sawa gari hilo na taratibu tukaanza kuondoka kuelekea getini. Mlinzi akafungua geti kisha tukaondoka, sasa hapo nikaanza kuliendesha gari hili kwa mwendo wa kasi sana kiasi cha kusababisha Latifa mara kadhaa kuguna na kunimbia kwamba niwe makini.

“Una namba ya Joseph?”
“Joseph yupi?”
“Yule wa ikulu, kitengo cha mawasiliano?”
“Ndio”
“Mpigie kisha nipe simu nizungumze naye”
Latifa akafanya kama nilivyo mueleza, baada ya simu kupokelewa akanikabidhi na kuiweka sikioni.
“Jose, nitumie namba ya raisi tena”
“Umeipoteza?”
“Hapana simu yangu imedumbukia kwenye maji”
“Sawa nakutumia”
“Asante kaka”
Nikakata simu na kuimrudishia Latifa simu yake.
“Sasa tunakwenda umefahamu wanahitaji ni wapi tuweze kuwakabidhi hizi nyaraka?”
“Ni wapi walikuambia?”
“Wameniambia tuonane Usagara kwa baba ubaya, tukifika hapo tuwapigie simu”
“Pao”
Nikazidi kuongeza mwendo wa gari ili kuhakikisha nusu saa linatukuta hapo sehemu ambayo tumelekezwa na majambazi hao. Ndani ya dakika ishirini na tano tayari tukawa tumesha fika kwenye eneo hilo. Latifa akaipiga namba ya simu ambayo alipigiwa nayo.

“Tumesha fikaa”
“Ohoo nimewaona, munaweza kushuka kwenye gari na kunifwata”
“Wewe upo kwa wapi?”
“Wewe shuka”
Niliweza kuyasikia mazungumzo yao, kutokana simu ya Latifa ina sauti kubwa kidogo, nikampokonya na kuiweka sikioni mwangu.
“Hatuwezi kushuka kwenye gari hadi tuweze kusikia sauti ya Luka”
“Ohoo kumbe, ok msikieni”
“Kakaaaa nakufaaa nisaidieniiii”
“Umemsikia”
“Ndio”
Meseji ikaingia kwenye simu ya Latifa kutoka kwa Joseph, ikanibidi kukata simu hiyo na kuipiga namba ya raisi.
“Dany unafanya nini?”
“Nazungumza na raisi kwanza”
Simu ya raisi ikaita kwa sekunde kadhaa kisha ikapokelewa.
“Habari mueshiwa, unazungumza na Agent Dany 008 kutoka NSS, tulizungumza asubihi kupitia namba yangu”
“Ndio ndio sauti yako kijana si rahisi kuweza kunipota masikioni mwangu”

“Sawa mkuu, vipi mpango si upo pale pale au kuma mabadiliko yoyote. Kwa maana nimeuliza hivyo kutokana simu yangu ya mkononi imeweza kuipata itilafu kidogo na namba hii ninayo itumia ni ya Agnet Latifa ambaye nimetoka naye kwenye kikosi kimoja”
“Mpango upo pale pale, sijabadilisha kitu, ila tayari amesha andaliwa mtu atakaye vaa sura yangu, na kuonekana kama mimi kwa hilo usijali”
“Sawa mkuu, huku viongozi wengi wapo kinyume na wewe mkuu. Ila nitahakikisha kwamba kila jambo linakwenda vizuri”
“Sawa kijana, saa nne usiku tutanza safari, nitakuja na walinzi wangu wawili ninao waamini”
“Sawa mkuu nitakupokea, na utakuwa unatumia namba hii kuwasiliana nami”
“Hakuna tatizo kijana”
Nikakata simu na kuirudisha kwa Latifa.
“Sasa unakwenda kuwakabidhi hizo nyaraka original?”
“Hakuna jinsi, nafanya yote haya kwa sababu Luka, mkewe ni mjamzito na anatakiwa kuweza kumuona mwanaye”
“Sawa”

“Wewe subiri kwenye gari, nipe simu yako, ila kuwa makini sana kwa kila kitu”
“Sawa Dany”
Nikaichukua simu yake, bastola mbili nikachomeka kwenye soksi kisha nikashuka kwenye gari nikiwa ninajiamini kupita maleezo. Nikaipiga tena namba ambayo tunatumia kuwasiliana na mtu huuyo.
“Njoo unaona hili geti jeusi”
Sauti hiyo ya Meya ikaniambia na kunifanya niangaze macho yangu kushoto na kulia, na kuliona geti jeusi kwenye upande wa kulia. Taratibu nikanza kulifwata huku sauti hiyo ya meya ikiniambia nizidi kusonga mbele taratibu. Nikafika hapo getini, nikashangaa kageti kadogo kakifunguka tu.
“Ingia”
Sauti ya meya ikaniambia kupitia simu. Nikaingia ndani  ya geti hilo, sikuamini macho yangu baada ya kukuta wasichana wapatao ishirini wakiwa wamevalia chupi pamoja na sidiria, wakiwa wamelizunguka swimming pool kubwa, huku pembeni kukiwa na vitanda vya kupumzikia vinne. Luka naye akiwa kwenye moja ya kitanda amejipumzisha huku wasichana wasili wakiwa wanamchezea kila sehemu.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )