Friday, March 9, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 31 na 32 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA                    
ILIPOISHIA      
“Sawa mkuu”  
Daktari akaongoza njia, tukafika hadi kwenye chumba ambacho ndipo madkatari wote wanapotakiwa kufika kazini asubuhi wanasaini na pale wanapo toka wana saidi. Raisi akaanza kuligagua daftari hilo, nikaona akitingisha kichwa tu.
“Naombeni koti na mimi leo niwe daktari nikaaa humu kuangali jinsi wanavyo kuja, nyinyi nilindeni kwa nje”
“Sawa mkuu”
Raisi akapewa koti la kidaktari kisha sisi tukatoka nnje ya chumba hichi kuendelea kuimarisha ulinzi. Muda wa kufika ofisini kwa mfanyakazi wa serikali mwisho ni saa moja na nusu tena kwa wale wa mbali ila hadi inafika saa mbili asubuhi hakuna hata mmoja aliye fika, jambo lililo nifanya niwaze sijui ni kitu gani watakacho fanywa na raisi hawa madaktari.

ENDELEA
Tukaanza kuona makundi makundi ya madakatari wakija huku wakitembea kwa mwnedo wa taratibu wakipiga stori kama vile wanakwenda harusini. Hapakuwa NA Daktari aliye weza kustukia ni kitu gani ambacho kinaendelea kwa wakati huu. Hadi wanaingia ofisini humo, ndipo hapo wengine wakagundua kwamba vibarua vyao vipo hatiani kufutwa. Madaktari na manesi si chini ya thelathini wote wamekuja nje ya muda wa kufika ofisini kama mfanyakazi wa uma.
Kutokana na wingi wa wafanyakazi hao hatukucheza mbali na raisi, ambaye amewaitisha kikao cha dharura ndani ya ofisi hiyo hiyo japo wote wamesimama.

“Nasemea kuanzia sasa hivi ninavyo zungumza, kazi hamuna”
Sura za manesi na madaktari zikabadilika kila mmoja aliweza kuweka pozi lake, mwenye machozi kumlenga lenga, yalimlenga lenga. Mwenye machozi kumtoka yakamtoka.
“Nyinyi munakuja kazini kama hospitali hii ni ya baba zenu na mama zenu. Daktari mkuu hapa ni nani?”
Mzee mmoja mweusi na mfupi akanyoosha mkono wa kulia.
“Hii hospitali kila mwaka inapata ruzuku ya kiasi gani kutoka serikali kuu?”
“Bilioni tano mkuu”
“Bilioni tano hizo zinatumika katika kufanya nini?”
“Kupaka rangi majengo na…..naa…..naaaaa…..”
Daktari huyo akapatwa na kigugumizi kizito cha kujibu dhairi hawa wanaonekana ndio walaji wa pesa za serikali.
“Hembu huyu muwekeni ndani akajibu hili swala takukuru”
Mlinzi aliyekuja na raisi akamtoa daktari huyo na kumpeleka kwneye magari tulio kuja nayo. Raisi akatoa simu yake na kupiga namba anazo zijua yeye.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )