Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, March 11, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 35 na 36 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA 
Nilizungumza hivyo huku nikishusha pumzi nyingi kwani ninahitaji kwenda kumtoa raisi kwenye gari aliloipo na kuondoka naye. Biyanka akaanza kufyatua risasi mfululizo, na kuwafanya washambuliaji kutulia kidogo, ikawa nafasi kwangu kukimbia hadi gari la raisi lilipo, kwa ishara nikamuomba afungue mlango wa gari lake kwa manaa pasipo yeye kuufungua kwa ndani mimi wa nje siwezi kuufungu. Raisi akafanya hivyo, japo ni jambo la hatari ila hakuna njia nyingine ya kufanya zaidi ya kufanya hivyo. Raisi akashuka huku kichwa akiwa amekiinamisha chini, nikaupitisha mkono wangu wa kulia kiunoni mwake, kitendo cha kugeuka na kumtazama K2 aliyopo upende wetu nyuma ya gari la raisi, nikakutana na uso wa bastola yake akiwa ameninyooshea mimi na raisi huku sura yake akiwa ameikunja akidhamiria kufanya hicho anacho kihitaji kukifanya kwa wakati huu.
      
ENDELEA  
K2 pasipo na huruma akafyatua risasi moja iliyo nifanya kuyafumba macho yangu nikiamini kabisa ninakufa kwa mkono wa K2. Ila sekunde kadhaa zikapita nikafumbua macho baada ya kuwana hakuna kitu ambacho kimetokea kwa upande wangu. Nikamtazama raisi na kumkuta akiwa yupo hai, nikamtazama K2 nikakakuta akiendelea kupambana na wavamizi hawa, nikatazama nyuma yangu, kwa umbali kidogo nikamuona mvamizi mmoja aliye valia nguo nyeusi na kinyago cheusi usoni mwake akiwa amelalal chini anamwagika damu za kichwa. 
 
Hapo ndipo nikaielewa lengo la K2, kuninyooshea bastola yake kwani ameyaokoa maisha yangu na kama sio hivyo basi ningekuwa nimesha kufa. Nikaongozona na raisi kwa mwendo wa haraka hadi kwenye gari letu. Raisi huyu ambaye ni feki na watu hawafahamu kwamba ni feki, akaingia kwenye gari nikamfungia mlango wa ndani. Tukaendelea kujibu mashabulizi huku kila mmoja jasho likimwagika kisawa sawa. Nikamuona K2 anaanza kupiga sarakasi za haraka hadi kwenye gari tulipo jificha mimi, raisi na Babyanka.

“Inabidi tuondoke hapa sasa hivi, watu wangu wote wamesha kufa”
K2 alizungumza huku akigema sana, kwani shuhuli tunayo ifanya sasa hivi sio ndogo, ni kufa na kupona pasipo kufanya hivyo basi maisha yetu yanakwenda kufa. Sote tukaingia kwenye gari huku nikijirusha kwenye siti ya dereva, kwa haraka haraka nikaanza kulirudisha gari nyuma huku risasi zikiendelea kurindima, kulifwata gari letu, cha kumshukuru Mungu gari yetu haiingii risasi na hii ndio pona pona yetu la sivyo miili yetu ingejaa risasi kutoka kwa wavamizi hawa. Nilaligeuza gari kwa kasi hiyo hiyo na likageukia kule tulipo tokea.

Nikakanyaga mafuta na kuanza kurudi tulipo tokea, ndani ya gari kila mtu akawa kimya nikamtazama raisi huyu feki nikamuona jinsi anavyo endelea kutemeka kwa woga. Tukiwa njiani tukapishana na gari za jeshi zikielekea eneo la tukio. Nikafika kwenye barabara ya bagamoyo inayo elekea Dar es Salaam, nikakunja kulia kwangu na kuendelea kuendesha kwa mwendo wa kasi japo nyuma yetu hakuna gari hata moja ambayo inatufukuzia.

    Masaa yakazidi kwenda mbio, hadi inatimu saa saba na nusu tukawa tumesha ingia jijini Dar es Salaam. Moja kwa moja tukaelekea ikulu, ambapo tukakuta pameimarishwa ulinzi mara dufu. Geti likafunguliwa baada ya askari kufika karibu ya gari letu, alipo muona raisi alituruhusu. Moja kwa moja nikaelekea kwenye maegesho ya gari za raisi. Tukashuka huku walinzi wengine wanne wakifika, karibu yetu nina imani taarifa ya kushambuliwa kwa msafara wa raisi ilisha tolewa ikulu. Moja kwa moja tukaelekea ndani na kumkuta raisi mwenyewe akiwa amesimama sebleni pamoja na viongozi wengine wakionekana wakiwa katika hali ya wasiwasi. K2 akastuka baada ya kumuona raisi halisi, aliye tufwata na kutupa mikono mimi na Babyanka.

“Hongereni sana vijana kwa kazi mulio ifanya”
“Asante muheshimiwa ni jukumu  letu”
“Pole bwana mdogo kwa kukuweka katika hali ya hatari”
“Ahaa kaka wewe acha tuu, wapo wapi wale madaktari wa kichina wanivue hii sura yako”
“Wapo watakuvuaa”
Raisi feki akaondoka na kuelekea katika vyumba vingine vilivyopo hapa ikulu na kutuacha na muheshimiwa raisi.
“Huyo ni mdogo wangu anaye nifwata mimi”
Raisi alizungumza huku akitutazama sisi, akatukaribisha na kukaa kwenye sofa za hapa sebleni, akawaomba viongozi wengine kuondoka akiwemo K2 ambaye hakujua ni mazungumzo gani muhimu ambayo mimi niliye chini yake nimebaki.

Baada ya mlango wa kutokea sebleni kufungwa raisi akashusha pumzi nyingi huku akitutazama kwenye nyuso zetu.
“Kimtazamo munaonekana kwamba mumechoka sana na pilika pilika za hapa na pale”

==>>Endelea Nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )