Wednesday, March 14, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 41 na 42 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA  

Rafiki yangu mmoja akagundua lugha yangu ya ukimya, taratibu akaanza kunisogelea na kukaa karibu yangu. Nikaitoa simu na kuiweka mezani, hata kabla ya huyu rafiki yangu kuishika simu ikaita na kujikuta sote wawili tukiitazama. Nikaipokea na kuongeza sauti ya kusikia hata aliyopo pembeni yangu anaweza kusikia kinachozungumza na mtu wa upande wa pili.
“Dany muda umeisha, nipo ripoti”  
“Sijafahamu alipo?”
“Ohoo ujinga wako ndio umekufanya usifahamu alipo Asma, basi ngoja nimtangulize Rose kuzimu”
Nikasikia mlio wa Risasi, na kuisikia sauti ya Diana akilia kwa uchungu.
“Kaka Dany….wame…muuaaa wifiiiii”
Nikaisikia sauti ya Diana akizungumza huku analia kwa uchungu sana, nikajikuta machozi yakinimwagika, hadi Khalid aliye kaa pembeni yangu akajawa na huzuni kubwa usoni mwake.

ENDELEA
Watu wote ndani ya ofisi wakatugeukia na kututazama mimi na Khalid, naamini ukimya wao waliweza kusikia mlio wa risasi katika simu yangu na sauti ya msichana akilia.
“Dan……”
Khalid akamkatisha Yohana kwa ishara ya mkono na kumuambia anyamaze na asizungumze chochote.
“Nakupa lisaa jengine mbele ukifanya mchezo, huyu mdogo wako naye anaondoka duniani”

Simu ikakatwa na kujikuta nikishusha pumzi nyingi nikiwa sifahamu nifanye nini kwa wakati huu. Marafiki zangu hawa wakajisogeza karibu yetu huku kila mmoja akihitaji kuweza kufahamu. Khalid akaanza kuzungumza kwa lugha ya vitendo na kuwaelezea tukio zima na kwamba simu hii hapa mezani ina vinasa sauti maalumu ambavyo tukizungumza tu basi majambazi walio mshikilia mdogo wangu watamuua. Kila mmoja mmoja akajitoa na kuahidi kunisaidia katika hili. Yohana akaleta laptop yake na kuiweka mezani kwangu. Akaitazama namba kisha akaiandika kwenye laptop, akaanza kuitafuta kwa kutumia Satelait, kila mmoja macho yake yapo kwenye kioo cha Laptop. Baada ya dakika mbili alamua  nyekundu ikatokea kwenye kioo huku ikiwa na ramani ya kutuielekeza ni wapi Yudia alipo na kundi lake. Uzuri ni hapa hapa Dar es Salaam.

Nikachukua karatasi na kuiweka mezani, kisha nikachukua na peni na kuandika maelezo yanayo wauliza wezangu ni nani anafahamu alipo Asma jambazi aliye kamatwa wiki moja iliyo pita.
Kila mtu akatingisha kichwa na kudai hafahamu ni wapi alipoa.
‘Dany cha msingi ni kumuokoa mdogo wako’
Yohana aliandika maandishi hayo kwenye laptop, nikatingisha kichwa na mimi nikaandika kwneye karatasi.
‘Hilo ndio jambo la muhimu, ila K2 asifahamu, baada ya hii kazi nitawaeleza kila kitu kinacho endelea kwa K2’
Kila mmoja akanitazama usoni akiwa na hamu ya kutamani kusikia ni kitu gani ambacho ninakifahamu juu ya K2. Nikasimama nikaichomoa bastola ya kiunoni mwangu, nikatoa magazine na kukuta risasi za kutosha nikaichomeka magazine tena, nikaiweka simu mfukoni.

Nikawapa ishara ya kutoka ofisini hapo mmoja baada ya mwengine ili kuto kustukiwa na mtu wa aina yoyote hata kama K2 akituona. Nikaanza kutembea kwenye kordo, nikafika sehemu ya lifti, nikafungua, nikaingia na kushuka chini. Nikamkuta Lucy akiwa amesimama sehemu ya maegesho ya magari lengo lake kubwa naamini kwamba ana nisubiria mimi.
“Dany”
Aliniita huku  akinifwata, nikasimama na kumsubiria hadi sehemu nilipo simama. Akanitazama kwa macho ya aibu.
“Zungumza nina haraka”
“Dany ninaomba tuweze kutoka Dinner?”
“Sina muda”
“Hata kama ni kesho au kesho kuwa”
“Baada ya hapo?”
Nilimuuliza Lucy swali hilo huku nikiwa na hasira, akabaki akinitazama usoni mwangu kwa maana hakutarajia kukutana na swali zito kama hilo.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )