Wednesday, March 21, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 53 na 54 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA   
ILIPOISHIA 
Monica akaondoka na kuingia jikoni, nikachukua simu na kumpigia mama.
“Nimeipata”      
“Ok kuna video ninakutumia, ipitie kisha uniambie tuisambaze au laa”
“Sawa mama unaitumia kwenye nini?”
“Kwenye emal yako”
“Ok”
Nikakata simu, kwa bahati nzuri hii sehemu kuna huduma ya inteenet ya bure, hazikupita hata dakika mbili email kutoka kwa mama ikaingia, nikaifungua email hiyo kisha video hiyo. Video hii inaonyesha K2 akiwa katika moja ya jengo kubwa ambapo humo ndani kuna kiwanda cha kutengeneza madawa ya kulevya jambo lililo nifanya nibaki nimeduwaa nisijue ni nini cha kufanya.
  
ENDELEA
Ikanibidi kuirudia tena video hii aliyo nitumia mama ambayo inaonyesha kama imerekodiwa na simu kwa maana mrekodiji mwenyewe mikono yake inacheza cheza. Uzuri wa mchukuaji video hiyo aliweza kuivuta sura K2 karibu sana.
Monica akarudi sebleni akiwa ameshika sahani yenye vipande vya kuku, akaviweka mezani huku akiitazama video hiyo.

“Huy…u si ndio yule aliye kuja kutuvamia na watu wake?”
“Ndio yeye”
“Hembu”
Monica akaigeuzia Laptop upande wake na kuitazama vizuri video hiyo, nikamuona anavyo shusha pumzi nyingi huku akinitazama usoni mwangu.
“Sasa hii video s uisambaze kwenye mitandao ajulikane kwamba yeye ni adui wa hii nchi kwa maana huu n unga kabisa wa kuvuta”
“Bado mapema, nahitaji ateseke kidogo kidogo hadi kufa kwake”
“Ila Dany hapo utakuwa unakosea, tazama maisha yetu kwa sasa yanavyo andamwa, afadhali mimi ninanafuu, wewe kila muda unatangaza kwenye vituo vya habari”
“Nimekuambia ninajua ni nini cha kufanya sawa”
Nilizungumza kwa ukali huku nikiifunga Laptop na Monica akatulia tuli. Ukimya ukatawala ndani ya chumba huku nikijaribu kuumiza akili juu ya kulipiza kisasi changu kwa K2 pamoja na kaka yake ambaye ndio raisi wa hii nchi. Monica akachukua kipande cha paja la kuku na kunilisha, sikuona hata ladha ya nyama hiyo japo ameipika vizuri sana.
“Usiku wa saa mbil tunaeleka Dar”
“Dar!!”
“Ndio, panga nguo zako na tunaondoka kama utakuwa tayari kuandamana na mimi katika hili”
“Sawa mimi sina tatizo”

Nikanyanyuka kwenye sofa na kuigia kwenye chumba, nikakisogelea kioo kilichopo humu ndani nikajitazama kuanzia chini hadi juu, nikatazama nguo za Monica alizo zimwaga kitandani pamoja na mawigi. Nikachukua moja ya gauni na kujipimisha kipimo cha mwili wangu, nikaona linananitosha.
“Ehee na hilo gauni unataka kufanya nini?”
“Nahitaji kulivaa, nataka uniweke na hili wigi”
“Hahahaaa Mungu wangu, Dany hembu acha vituko vyako”
“Vituko vya nini sasa, nahitaji kubadilika muonekano niwe mtoto wa kike, kuna watu wangu kupitia muonekano huu nitaweza kuwapata”
“Mmmm hembu livae nikuone”
Nikavua nguo zangu na kubakiwa na tisheti pamoja na boksa, nikalivaa gauni hil jeusi lililo jaa vimetometo vya dhahabu.
“Waoooo it’s so amaizing”
Monica alizungumza huku akinisogelea, akanifunga zipu kwa nyuma, kwa jinsi nilivyo nyoa upara na ndevu si rahisi mara moja kwa mtu kunigundua kwamba mimi ni mwanaume pale nitakapo vaa wigi.

==>Endelea Nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )