Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, March 22, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 55 na 56 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA  

Nikanyanyuka huku nikiwa nimeushika mkono wa mama Mariam, nikasogea taratibu hadi sehemu alipo simama mama Mariam, neneja huyo akanitazama kwa macho ya dharau huku akinipandisha na kunishusha na macho yake.
“Na wewe dada mzima unamtongoza jimama kama hili, unataka mukasaganeee eheee?”
Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama meneja huyu.
“Nakuuliza usinikodolee macho kama umechomekwa mbo** ya mkund………”
Sikumruhusu kumalizia sentensi yake, nikamtandika ngumi ya pua, iliyo muangusha chini mzima mzima na kutoa kishindo kizito hadi wapishi wwalipo jikoni wakatoa kushangaa ni kitu gani kinacho endelea huku nje.
  
ENDELEA
“Uwe na adamu na wanawake unao waona, pumbavu wewe”
Nilizungumza kwa sauti ya kike ila yenye kijiujazo kwa mbali hadi mama Mariam akanitazama usoni mwangu. Meneja huyo akajizoa zoa na kunanyuka huku akijifuta futa vumbi kililo jaa kwenye suti yake, hakuna mtu aliye msemesha zaidi ya kubaki kumuangalia, taratibu akaondoka akiwa apole kama sio yeye aliye kuja akitukana matusi mfululizo kwetu.
“Asante sana binti ila mimi kwangu kibarua ndio kimekwenda na maji”
“Usjali, hakuna jambo kama hilo”
“Mmmm”
“Yaa niamini mimi”
Nikjitahi kuzungumza kwa sauti ya kike ili mama Mariam asinifahamu kabisa kwa maana kunifahamu kwake inaweza ikawa ni tatizo jingine kwa maana bado siweza kumuamini mara moja isitoshe nipo kwenye tatizo kubwa kama hili la kutafutwa nchi nzima kama gaidi.

“Naomba unitengenezee juisi na uniletee katika chumba changu”
“Juisi gani?”
“Juisi ya parachichini lililo changanywa na pensheni.”
Nikamtajia namba ya chumba mama Marimu kisha nikampa shiling elfu hamsini.
“Ya nini hii?”
“Kwa ajili ya usumbufu wa kuniletea juisi hiyo chumbani kwangu, nahitaji jagi zima”
“Sawa binti”
Nikaondokea huku nikitamani kuangalia nyuma kumuangalia mama Mariam ila nikashindwa, nikapanda gorofani kwa kutumia lfti, nilipo fika katika mlango wa chumba changu nikabisha hodi, Monica akanifungulia mlango na nikaingia ndani.
“Mbona umechelewa honey?”
“Nilikuwa natoa maelekezo kwa wapishi”
“Ahaa sawa”

Nikapanda kitandani huku nikiwa nimeshika rimoti ya Tv, niliyo ichukua mkononi mwa Monica, nikaanza kubadilisha chaneli moja baada ya nyingine, kuangalia ni kitu gani ambacho kinaendelea. Hapakuwa na jambo jipya zaidi ya picha yangu kutangazwa. Mlio wa simu ya Monica ndio ulio nifanya niweze kumgeukia na kumtazama, akanitazama machoni kisha akaipokesa simu yake.
“Halooo”
“Nini?”
“Ohooo Mungu wangu, jamanii”
“Ok ok”
Monica alizungumza huku akiwa amebadilika na kuchanganykiwa, wala sikufahamu ni jambo gani ambalo linamsumbua. Akakata simu na kuiweka pembeni na kuanza kumwagika na machozi, ikanibidi kumvuta karibu yangu na kumkumbatia
“Honey kuna kitu gani kilicho tokea”
“Ni mdogo wangu ohoooo Mungu wanguu jamani weeee”
“Mdogo wako amepatwa na nini?”

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )