Monday, March 26, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 63 na 64 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA-
ILIPOISHIA 

Nikafika katika hoteli ya Serena, walinzi wa getini walipo ona namba za gari langu hawakuhitaji kulikagua sana, nilicho kifanya ni kipita na kulisimamisha kwenye maegesho ya magari. Nikaacha bastola moja chini ya siti ya gari, nikajiweka vizuzri kofia yangu, hata sura yangu haikuonekana vizuri.
Nikashika kitasa cha mlango wa gari langu, kabla sijaufungua nikamuona K2 akitoka na mzee niliye mfwata wakaingia naye kwenye gari kisha wakaanza kuondoka jambo lililo nifanya nibaki nimeduwaa nisijue ninaanzia wapi kwa maana gari si chini ya nne zimeongozana na gari la K2 na zote zinatoka katika ofisi za N.S.S(Nation Securty Service)

ENDELEA  
Taratibu nikawasha gari langu na kuanza kuzifwatilia gari hizo huku nikiwa nimeziacha kwa umbali mrefu kidogo. Nikatoa simu mfukoni na kumpigia Babyanka ambaye alisha iingiza namba yake kwenye simu yangu.

“Ndio Dany?”
“Dili limeharibika”
“Kwa nini?”
“Kipindi ninafika tu, nimekuta K2 anatoka na mzee yule wa Kimarekani”
“Ohoo Gody sasa inakuwaje?”
“Hapo ndio ninaumiza kichwa kufikiria ninafanyaje kwa maana wana msafara wa gari kama nne hivi na zote zimetoka katika kitengo cha N.S.S.
“Mmmm kwa sasa wanaelekea maeneo ya wapi?”
“Maeneo ya Mwenge”
“Mwenge Mwenge…..”
“Hembu usikate simu nimpigie mama atushauri juu ya hili swala tufahamu ni nini cha kufanya”
“Sawa”
Nikaingiza namba ya mama kwa haraka kisha nikampigia, simu ya mama haikumaliza hata sekunde tano kuita ikapokelewa.
“Mama kuna tatizo”
“Tatizo gani?”
“Huyu mkuu wa watu wanao husika katika kuibinafsisha nchi yupo mkononi mwa K2 na hapa ninavyo zungumza nimeongozana nao na sifahamu wanampelekea wapi?”
“Upo eneo gani?”

“Tunaelekea Mwenge huku”
“Mwalimu”
“Kumbe Babyanka yupo”
“Ndio mwalimu, mimi nipo nyumbani ila unaonaje kama tukazi control trafick Light?”
“Wazo zuri, Dany munatokea upande gani?”
“Upande wa huku Morocco”
“Ok nafungulia gari zinazo toka Mlimani kuelekea Mbezi  Beach, nitawasimamisha hapo kwa dakika kum na tano, Dany hakikisha kwamba hii kazi unaifanya vizuri”
“Sawa mama”
“Dany mimi ninaelekea ofisini”
“Sawa”
Nikakata simu na nikaiweka pembeni, nikaanza kuyapita magri yaliyopo mbele yangu hadi gari za N.S.S. Lengo langu kubwa ni kuiwahi foleni na ninahitaji gari langu kuwa la kwanza. Kama nilivyo panga nivyo ilivyo kuwa. Nilipo fika tu kwenye foleni taa za kusimamisha magari upande wetu zikawaka na kufanya magairi yote kusimama.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )