Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, March 5, 2018

Ajali Ya Basi New Force Na Basi Dogo Toyota Hiache Yasababisha Vifo Vya Watu Watano

adv1
WATU watano wakiwemo wanawake wanne na mwanaume mmoja ambaye ni dereva basi ndogo aina ya Toyota Hiache yenye namba za usajili T 962 BSE aliyetambuliwa kwa jina la Jackson Adam wamefariki dunia papo hapo baada yakugongana na basi  la  New force New lenye namba T 346 DLY likitokea  Dar es Salaam kuelekea Tunduma na kusababisha majeruhi  ya watu wengine tisa na kulazwa  hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibisha kutokea kwa ajali hiyo  Machi 4, mwaka huu majira ya saa nne asubuhi  katika barabara kuu ya Morogoro – Iringa  eneo la Lungemba – Rombo , Manispaa ya Morogoro kwa kuhusisha basi la aina ya Youtong  lenye namba za usajili T 346 DLY mali ya kampuni ya New force.

Basi hilo lilikuwa likitokea   Dar es Salaam kwenda Tunduma  na lilipofika eneo hilo liligongana uso kwa uso na basi ndogo  aina ya Toyota Hiache yenye namba za usajili T 962 BSE ambayo lilikuwa likitokea kijiji cha   Mlali, katika wilaya ya Mvomero kwenda Morogoro Mjini.

Kamanda Matei alisema katika ajali hiyo  abiria  watano waliokuwa ndani ya Toyota Hiache walifariki dunia papo hapo na wengine  tisa kujeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Morogoro  kwa ajili ya kupatiwa matibabu na hakukuwa na majeruhi kutoka  basi la New Force .

Kamanda wa Polisi wa huyo aliwataja waliofariki dunia ni pamoja na dereva wa basi dogo  Jackson Adam ambaye ni mkazi wa Kata ya Chamwino, Manispaa ya Morogoro,  na wengine wanawake Georgina Aloyce (35) , Revocatha Raymond Lyimo , Mangasa Almasi  na Witness Leonard Mwamuni (26).

Pia aliwataja majeruhi waliokuwa kwenye  basi dogo ni  watoto wawili waliofiwa na mama yao katika   ajali hiyo ambao ni Catharine Mhagama (6) na Caltimei Mhangama  mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili, Prisca Isaya (25), Chuki Wage (40), Anthon Cletus Mhando (39) mkazi wa eneo la SUA, Innocent Emilian , Willbrod Emilian ambao ni watu wazima mapacha , Iman Amri  Salum  na kondakta wa daladala hiyo  Ally Ramadhan.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi huyo  , chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi dogo ambaye ni marehemu kutaka kulipita lori la mchanga lililokuwa mbele  yake bila kuchukua tahadhari na hivyo kugonaga na basi la Kampuni ya New Force ambalo lilikuwa likiendeshwa na Mdula   Abdallah  (52) mkazi wa Dar es Salaam. Hata hivyo alisema , Polisi inamshirikia dereva  Mdula Abdallah wa Kampuni ya New Force kwa ajili ya uchunguzi zaidi  kutokana na ajali hiyo.

Alisema ,mazingira ya ajali hiyo inaonesha  huenda dereva wa basi hilo alikuwa katika mwendo kasi uliomsababishia ashindwe  kupunguza mwendo mara baada ya kuona  basi ndogo likilipita lori lililokuwa mbele ambapo ageweza   kunusuru ajali hiyo mbaya iliyopoteza maisha ya watu isitokee
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )