Tuesday, March 27, 2018

Aliyemnajisi mtoto wake hadi kifo, apewa shtaka la mauaji

Mtoto Mase Denis kutoka Kabwana wilayani Rorya mkoani Mara aliyedaiwa kunajisiwa na baba yake wa kufikia Machi 3, mwaka huu alifariki dunia wakati akiwa njiani kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Rufani Bugando jijini Mwanza juzi.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime-Rorya, Henry Mwaibambe aliwaambia waandishi wa habari kuwa awali mtuhumiwa Denis Ondigo alishitakiwa kwa kunajisi lakini kutokana na kifo hicho amebadilishiwa kuwa shtaka la mauaji.

Mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo majira ya saa 6 mchana wa Machi 3 akiwa nyumbani kwake Kabwana  baada ya mama wa mtoto kuwa amekwenda dukani kununua mahitaji ya nyumbani.

Kamanda huyo alisema Ondigo (26) mkazi wa Kabwana alifikishwa Mahakama ya Wilaya Tarime mkoani Mara kwa mara ya kwanza Machi 13.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )