Wednesday, March 28, 2018

Barakah The Prince aweka wazi sababu ya bifu lake na Nay Wamitego

Mwanamuziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amefunguka na kuweka wazi kilicho sababisha kuwepo kwa ugomvi  kati yake na msanii mwenzake Ney wa Mitego.

Sakata hilo lilianza baada ya Nay wa Mitego kumchana Barakah kwenye wimbo wake uitwao ‘Moto’ aliouachia  mwaka jana mwezi Julai ambapo kwenye wimbo huo Nay aliimba; Itafika hatua tuchangishane elfu hamsini tuwarudishe wadogo zetu Mwanza akamtaja Barakah the Prince.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Jembe Fm, Barakah amefunguka na kusema kisa cha Nay kumuimba vile ni baada ya yeye kumchana na kumwambia kipaji chake cha kurap ni kidogo:

"Nay wa Mitego mimi nilishawahi kumwambia studio kwake kwamba wewe sio rapa mkali .Nilitoka studio nikamkuta [Nay] anadiss kuhusu Godzilla, mimi nikamwangalia nikamwambia huyu jamaa mbona kipaji chake kidogo sana.

"Ujue Godzilla ni rapa sasa wewe Nay Wamitego unarap kitu gani? Haumfikii Godzilla hata kidogo, wewe ni msanii unaunga unga. Hapo ndipo alipopaniki akaamua kwenda kuniimba, siwezi kumjibu mtu ambaye hana kipaji”.
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )