Friday, March 16, 2018

Harmorapa: Albamu Ya Diamond Mbaya Kama Sura Yangu

Msanii wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Harmorapa ameibuka na kuiponda Albamu ya Diamond na kudai ni mbaya kama ilivyo sura yake.

Harmorapa alijipatia umaarufu kwa kupenda kiki katika maswali kadhaa kuliko muziki wake na leo ameibuka na jipya kuhusu Albamu mpya msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Albamu ya Diamond inayoitwa ‘A boy from Tandale’ imetoka rasmi jana usiku ambapo ilifanyiwa uzinduzi rasmi nchini Kenya.

Harmorapa kupitia ukurasa wake wa Instagram ameinanga Albamu ya Diamond na kudai ameitangaza sana alafu ametoa kitu kibovu:

"Bro Chibu naye kelele nyingi za Albamu miezi saba mwisho wa siku anatutolea albamu mbovu kama sura yangu sokwe, cha kukushauri Simba kama mkataba wako wa karanga umeisha kaa dukani kwa dada yako Esma umsaidie kuuza vitenge”.

Lakini Harmorapa amejitamba na kudai kuwa albamu yake ambayo atakuja kuitoa itakayoitwa Uthigawepathi itakuwa kali kuliko hiyo lakini pia amesema albamu ya Ali Kiba itafunika kupita maelezo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )