Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, March 19, 2018

Harmorapa Amtolea Povu Uchebe na Kudai Ameolewa na Shilole

Rapa wa muziki wa Bongo fleva Harmorapa aliyejipatia umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii kwa vituko vyake amerudi tena  na safari hii yuko na Shilole pamoja na mumewe Uchebe.

Harmorapa ameibuka na kudai kuwa Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole amemuoa mumewe Uchebe. Huku akidai kuwa kitendo cha Uchebe kuacha kazi yake ya ufundi gereji na kumtegemea mke wake ni sawa na kuoelewa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmorapa amerusha dongo hili lililowaelekea Uchebe na Shilole:

"Uchebe mtoto wa kiume umeacha Kupiga  spana umekimbilia Kuolewa. Kwa nini badgirlshishi akuosheshe vyombo? Uchebe mtoto wa kiume rudi gereji ukapige spana la sivyo utapigwa sana vibao na shishi na kufulishwa mpaka chup*, sura yenyewe imekukunjika kama yangu utafikiri tumetoroka kwenye zui la manyani/ hiyo ndio faida ya wanaume marioo vibenteni demu wanahudumia masponsa mzigo tunakula sisi kimya kimya na chup* tunachafua sisi wahudumiaji alafu  vibenteni kama Uchebe kazi yao kutakatisha chup*”.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa mwaka jana mwishoni, kabla hawajaoana Uchebe alikuwa fundi magari gereji lakini baada ya kufunga ndoa amekuwa akionekana kila mahali na Shilole akimsindikiza kwenye shoo zake zote hali iliyozua maneno maneno.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )