Saturday, March 17, 2018

Jakaya Kikwete Alipongeza Jeshi la Polisi


Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefunguka na kulipongeza jeshi la polisi Tanzania kwa kuweza kufanikisha kukamatwa kwa watu ambao walikuwa wakitumia vibaya majina yake, mkewe na mtoto wake kuwaibia watanzania.

"Natoa pongezi nyingi kwa IGP Simon Sirro na Polisi Tanzania kwa kuwakamata watu waliokuwa wanatumia vibaya jina langu, la mke wangu Salma na mwanetu Ridhiwani kuwahadaa na kuwaibia Watanzania ninaowapenda sana. Kubainika kwa mtandao huo na kukamatwa ni hatua nzuri ya kupongezwa" alisema Jakaya Kikwete

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa watu hao ambao wamekamatwa na jeshi hilo la polisi watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )