Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, March 25, 2018

Jeshi la Polisi Mwanza Latoa ONYO Kali kwa Wanaohamashana Kuandamana

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza  limewaonya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaotumia vibaya mitandao hiyo kufanya uhalifu ikiwemo kuhamasisha maandamano haramu
 
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Naibu Kamishina Ahmed Msangi ametoa onyo hilo hii  jana wakati akizungumza na askari waliokuwa kwenye mazoezi mbalimbali yaliyofanyika katika uwanja wa polisi Mabatini Jijini Mwanza.

RPC Ahmed Msangi alisema; "Kuna watu wanapeana vihabari vya kwenye mitandao ya kijamii wafanye uhalifu na uhalifu wenyewe ni wa kufanya maandamano au mkutano usiokuwa na taarifa na kiukweli imepigwa marufuku"

Aidha, RPC Msangi wamewataka Polisi kufanya uchunguzi ili kuwabaini wanaoshinikiza hayo na kisha kuwahoji na kujua nia yao ya kutaka kufanya hivyo ni ipi

Baadhi ya askari walioshiriki mazoezi hayo wameeleza kwamba yanawasaidia kuwa imara wakati wote na hivyo kutimiza vyema majukumu yao.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )