Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, March 5, 2018

Kabla Sijafa - Sehemu ya 05( Simulizi ya Kweli)

 Mwandishi: Grace G. Rweyemam

Nilikupenda Marietha mke wangu, kwa moyo wangu wote, na hakuwahi kutokea mwanamke bora zaidi yako, ila niliufumba ufahamu wangu kuona uzuri wa moyo wako pindi uliponikosea.

 Asilimia ishirini nilizokosa kwako zilinifanya kusahau asilimia themanini ulizonipa, za upendo na uzuri wa moyo wako. Nilisahau kuwa mara nyingi nimekuwa nikikukosea, ukanisamehe bure kabisa. Nilipoumizwa uliponinunia, nilitafuta kukukomoa, lakini sikujua ninatengeneza bomu la kuilipua familia yangu yote. Umenifundisha upendo wa kweli ni nini, lakini sikukubali kushika agano nililoliweka mbele ya Mungu na watu.

Sitamani mwanaume yeyote, na wala mwanamke, afanye kosa nililofanya au linalofanana na hilo. Ni vema kuzungumza na kutafuta muafaka unapokosewa au unapokosana na mwenzako, kuliko kutafuta amani kwingine popote.

Wenzi tulionao ni wazuri, ila madhaifu yao kidogo hufumba macho yetu tusione uzuri wao. Maana halisi ya ndoa ni kumkubali mwenzi wako, kumpenda, na kuwa mwaminifu kwake, hata wakati ambapo unahisi amekuudhi.

Uaminifu ni ngao kubwa mno kwa ndoa imara. Ninaomba unisamehe mke wangu, kwa kuyajua haya yote nikiwa nimechelewa kabisa. Natamani dawa ya UKIMWI igundulike ya kumtibu mtu mmoja tu, na mtu huyo awe wewe malkia wangu.

Nisamehe kwa kukunyima haki yako ya kuwa mama mpaka uzee wako, nisamehe kwa kukupunguzia miaka ya kuishi, nisamehe kwa kukatiza ndoto zako, nisamehe kwa kukatiza miaka yangu ya kuwa baba kwa watoto wako, nisamehe kwa kuwafanya wanao kuwa yatima kabla ya wakati, nisamehe kwa kuuumiza moyo wako na kuvunja imani uliyonipa, nisamehe hata kwa kuja kwenye maisha yako, kwani usingekubali kuolewa na mimi leo hii ungekuwa mwanamke mwenye furaha zaidi na maisha marefu.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )