Monday, March 26, 2018

Kauli ya Kwanza ya Abdul Nondo Baada ya Kuachiwa kwa Dhamana

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) Abdul Nondo kwa mra ya kwanza amefunguka na kuwashukuru watanzania baada ya kuachiwa kwa dhamana katika mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Iringa leo Machi 26, 2018

Nondo ameweka wazi hayo baada ya kuachiwa huru na kusema kuwa sasa anaweza kuendelea na masomo yake pamoja na kesi hiyo ambayo itakuwa ikiendelea mkoani Iringa.

"Namshukuru sana wakili Jebra Kombole na wakili wangu mwingine wa Iringa mbali na hapo napenda kuwashukuru wadhamini wangu kwa sababu masharti ya dhamana yalikuwa yanahitaji wadhamini kutoka mkoa wa Iringa kwa hiyo nimepata wadhamini mkoa wa Iringa Mungu awabariki sana.

"Saizi nipo huru naweza kwenda kuendelea na chuo huku nikiendelea na kesi mkoa wa Iringa. 

"Pia nawashukuru Afisa Magereza kwenye eneo ambalo nilikuwa nikiishi katika kusubiria dhamana wamenitunza vizuri kwa upendo na ushirikiano mkubwa hivyo nawashukuru wazazi wangu na Watanzania Mungu awabariki sina zaidi ya zaidi ya hayo" alisema Nondo

Kesi ya Abdul Nondo itatajwa tena tarehe 10 mwezi wa nne mwaka huu mkoani Iringa ambapo wataanza kusikiliza hoja za awali, wakili wa Nondo amewataka watanzani kuwa na subira juu ya jambo hilo kwa kuwa tayari lipo mahakamani hivyo litafahamika.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )