Thursday, March 8, 2018

Leo ni Siku ya Wanawake Duniani.....Tazama Hapa Alichokisema Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 8, 2018 katika siku ya wanawake duniani amefunguka na kuwapongeza wanawake wote wa Tanzania na kuwatakia kheri katika siku yao hii muhimu.

Magufuli ametoa ujumbe huo kupitia mtandao wake wa twitter na kusema kuwa wanawake wamekuwa na mchango mkubwa sana katika jamii na kusema daima ataendelea kuwaheshimu

"Nawapongeza wanawake wote kwa kusherehekea siku yenu ya leo na hasa kwa mchango wenu mkubwa mnaoutoa kwa jamii. Daima tutaendelea kuwaheshimu, kuwapa ushirikiano na kutambua juhudi zenu katika kujenga ustawi wa jamii yetu" alisema Rais Magufuli

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )