Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, March 23, 2018

Lulu Diva: "Msinifananishe na Shilole"

adv1
Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya muziki wa mduara Lulu Diva ‘Diva Divana’ ameibuka na kusema hataki kufananishwa na msanii mwenzake Shilole.

Lulu Diva amewataka mashabiki ambao wanafananisha rekodi zake na na miondoko ya nyimbo za Shilole waache kumpambanisha naye kwani hataki beef naye.

Lulu Diva amefunguka hayo Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, ambapo amedai anamheshimu Shilole kama dada yake hivyo hatopenda kuwa na beef naye:

"Hapana Jamani hakuna mtu ambaye anapotezwa kila mmoja anaimba mziki wake na mimi Shilole namheshimu kama dada na anafanya mziki wake wa kwake peke yake yaani hata ukiangalia mziki anaofanya na mziki wangu ni vitu viwili tofauti ni watu tu wanatengeneza vitu ili waweze kutuchonganisha”.

Lulu Diva aliendelea kumwagia Sifa Shilole huku akisisitiza hataki bifu naye:

"No mimi namheshimu sana as a sister she is a legend,ameanza mziki kabla yangu, anajua vitu vingi kwenye gemu kabla yangu.... kwaiyo wasitengeneze hiyo kitu mpaka mimi nikawa kuna kitu nataka kujua kuhusu mziki nikashindwa kumfuata kwa sababu ya maneno, kwaiyo naomba hivyo vitu visiwepo mimi nafanya mziki wangu mimi kama mimi”.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )