Sunday, March 25, 2018

Majambazi Yafunga Barabara na Kuteka Magari Pwani...Mawili Yatiwa Mbaroni

JESHI la polisi mkoani Pwani, linawashikilia watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi kati ya kundi la majambazi zaidi ya sita ambao waliteka magari na kupora mali mbalimbali za watu eneo la Kwang’andu ,Mbwewe barabara ya kuelekea Wami.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani,(ACP) Jonathan Shanna alisema tukio hilo limetokea machi 24 saa 8.30 mchana .


Akizungumzia tukio hilo la unyanga’anyi wa kutumia silaha ,alieleza majambazi zaidi ya sita waliteka magari kwa kukata mti kwa msumeno kisha kuziba barabara na kuvamia magari mbalimbali ya wananchi kisha kuwapora mali zao na kuharibu baadhi ya magari yao.

Aidha kamanda Shanna alisema, watuhumiwa wawili wapo mbaroni kupisha uchunguzi.Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Saidi Salim (26) na Nyangwesa Nyangwesa.


Kamanda Shanna aliwataja na wananchi /wasafiri walioharibiwa na kuporwa mali zao akiwemo Peter Kilango, ambae aliporwa simu aina ya techno C9 na gari lake kuharibiwa kioo cha mbele upande wa dereva.

Viatus Bahati aliporwa Lap Top Dell, Usd 900.00 , shilingi 700,000 na pochi yenye document mbalimbali na Imail Meshileki alieporwa simu aina ya Tecno ,na sh .800,000 na gari lake  T.953 BXN Toyota Prado ambayo waliiharibu kioo cha nyuma.

Kamanda Shanna alimtaja mwingine ni Jackson Omary aliyeporwa Tsh.70,000 na begi lenye nguo mbalimbali na Denis Mwavano aliporwa simu Tecno C9.

Jeshi la polisi mkoani humo limekemea vitendo vya kiuhalifu na kuteka magari kwani kwa kufanya hivyo watakula nao sahani moja ,na wale waliofanikiwa kukimbia wataendelea kusakwa
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )