Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, March 12, 2018

Aliyemtaja Mange Kimambi, Zitto Kabwe, Tundu Lissu na wengine kuwa ni watu 10 hatari zaidi Tanzania kuburuzwa mahakamani

adv1
Mjasiriamali/Mwanahabari na Mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi amefungua kesi ya madai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Mhariri wa Gazeti la Tanzanite na Mwanasheria Cyprian Musiba kwa kumkashifu na kuchafua jina lake kupitia mkutano wake na Waandishi wa Habari uliyofanyika tarehe 25 Februari, 2018.

Barua hiyo iliyotolewa na Mwanasheria wa Maria Sarungi, Benedict Alex Ishabakaki imeeleza kuwa mteja wake alitajwa na gazeti la Tanzanite toleo Namba 50 lililotoka Februari 26, 2018 kuwa ni moja ya watu hatari kwenye usalama wa taifa.

Kwa upande mwingine, barua hiyo imeitaka  Dar24 kufuta habari hiyo na kuomba radhi hadharani kwa kitendo cha kuandika habari hiyo yenye lengo la kumfedhehesha mteja wao.


adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )