Tuesday, March 27, 2018

Mrembo Aibuka na Kudai Aliahidiwa Ndoa na Diamond

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amekuwa akitawala headlines za social media tangu aachane na aliyekuwa mpenzi wake Zari.

Wiki chache zilizopita Diamond alitangaza nia yake ya kutaka kuoa mwaka huu lakini hakuweka wazi atamuoa nani huku kila mwanamke wake wa zamani akitajwa katika nafasi hiyo.

Mrembo anayejulikana kwa jina la Rehema Fabian ambaye aliwahi kushiriki kinyang’anyiro cha Miss Kiswahili 2009, ameibuka na kudai alikuwa na historia ndefu na Diamond kuliko wanawake wengine wote.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda Rehema alisema kuwa, amesikia kuhusu Diamond kutangaza kuwa atafunga ndoa mwezi wa sita mwaka huu, lakini ni vyema Watanzania wakajua kwamba yeye na Diamond walikuwa ni wapenzi wakati msanii huyo anatoka kwa mara ya kwanza.

"Nimesikia kuwa Diamond anataka kuoa mwezi wa sita, natamani nijue anamuoa nani kwa sababu wengi tuliahidiwa kuolewa, lakini mwisho wa siku tulibwagwa, mimi ndiye msichana wa kwanza kabisa kuwa na staa huyo wakati anapata tuzo ya kwanza ya MAMA ambayo aliipatia nchini Nigeria na nilikuwa na mchango mkubwa katika kupata kwake mafanikio”.

Rehema aliendelea kufunguka kuwa, ameamua kusema haya kwa sababu Diamond hajawahi kumtaja popote kuwa alikuwa na uhusiano naye wakati yeye ndiye wa kwanza na katika mafanikio yake amechangia kwa kiasi kikubwa.

Rehema aliweka wazi kuwa sababu iliyopelekea wao kuachana ni Diamond kuchepuka na Wema na kuanzisha Mahusiano naye jambo alilodai lilimuumiza sana na aliweka wazi kuwa alikesha usiku na mchana anaomba waachane.

Lakini pia Rehema alimtaka Diamond kabla hajaoa akumbuke fadhila zake na aeleze umma ukweli wa penzi lao ili kufuta kile alichonacho moyoni kwani alitarajia baada ya kuwa na mafanikio, angemtafuta angalau kula naye bata, lakini hakuwahi kufanya hivyo ingawa alimuahidi mambo mengi mwanzo wa kusaka mafanikio.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )