Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, March 9, 2018

Mrembo Aliyedaiwa Kuolewa na Alikiba Afungukia Tuhuma Hizo

adv1
Video vixen maarufu kutoka nchini Kenya anayejulikana kama Tanasha  Donna Barbieri Oketch ‘Zahara Zahire’ ambaye alionekana kwenye video ya wimbo wa Alikiba na Christian Bella ‘Nagharamia’ amekataa kuwa na uhusiano na Alikiba.

Kwa wiki sasa kumekuwa na taarifa zilizokuwa zinaenea mtandaoni ambazo zinadai kuwa supastaa huyo wa Bongo fleva Alikiba anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni lakini tatizo likawa bibi harusi hajulikani ni nani.

Lakini mara moja habari zilianza kuenea kuwa mrembo ambaye anatarajiwa kuolewa na Alikiba ni mkenya anayeishi Moombasa na baadae kuja kusikika bibi harusi ni Tanasha.

Tanasha amejitokeza na kukataa kata kata taarifa hizo za kuolewa na Alikiba wala kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi. Tanasha aliweka wazi ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa SnapChat ambapo aliandika;

Kwenye ujumbe huo Tanasha ameelezea kuwa taarifa zinaoenea kwenye mitandao Tanzania kuwa ana uhusiano na Alikiba ni za uongo na uzushi na kudai aliwahi kutokea kwenye video yake moja tu ya wimbo wake lakini hawajawahi kuwa wapenzi.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )