Friday, March 23, 2018

Nafasi Ya Uchawi Kwenye Kamali

NAFASI   YA   UCHAWI   KWENYE   KAMALI
NA.  DOKTA  MUNGWA  KABILI…0744  000  473.

=============================================================
Watu mbalimbali  wamekuwa  wakitaka  kujua  maoni  yangu  kuhusu  nafasi  ya  uchawi  kwenye  kamali  na  michezo  ya  bahati  nasibu.  Yafuatayo  ndio  maoni yangu.

Toka  enzi  na  enzi  watu  wamekuwa  wakitumia  uchawi  ili kupata ushindi katika   kamali  na  katika  hilo  zimekuwa  zikitumika  kila  aina  ya  ndumba za kichawi   kuanzia  wale  walio  tumia  mashimo  ya  Nyegere, mafuta  ya  usiku, Pete za  bahati, Ngekewa,  Ndagu, sungura  weupe  nakadhalika nakadhalika.

Uchawi  una  nafasi  kubwa  sana  katika  kamali.  Maisha  ya  wacheza  kamali  mahali  popote  duniani  hutawaliwa  na  uchawi.

Uchawi  huanza  kutawala  maisha  ya  mcheza  kamali  kuanzia  siku  anapo  anza  rasmi  kucheza  kamali  mpaka  siku  atakayo  ingia  kaburini.

Uchawi  huwatawala  wacheza  kamali   wakiwa  duniani  n ahata   baada  ya  kuondoka duniani.

Ninasema  hivyo  kwa  sababu, moja  kati  ya  ndumba  zenye  nguvu  sana  katika  kamali  ni  zile  zinazo  tokana  ama  kutayarishwa  kwa  kutumia  makaburi  ya  wacheza  kamali  mashuhuri.  Wacheza  kamali  ninao  wazungumzia  hapa  ni  wale  ambao  waliyatoa   na  kuyatumia  maisha  yao yote  kwenye  mchezo  wa  kamali.

Kwa  mtu  ambae  alitajirika  kupitia  Kamari, kaburi  lake  huwa  lulu  yenye  thamani  kubwa  sana  katika  uchawi  wa  kamali . Watu hutumia  kaburi hilo  kutengeneza  ndumba  kwa  ajili  ya  kupata  mali  na  utajiri  kwa  njia  ya  kamali. Ndumba  hizo  huwasaidia  kushinda  kwenye  kamali.

Kwa  watu wengi  wanapo sikia  kuhusu  uchawi  wa  makaburini, akili  zao  moja  kwa  moja  huwa  zinaenda  kwenye  uchawi  wa  kuzika  nyota  za  watu, kuzika  kesi, kuzika  ndoa, mahusiano, biashara  za  watu , kuwatia  watu  nuksi, mabalaa  na  mikosi  nakadhalika.

Wasicho  kifahamu  ni  kwamba, makaburi  yanaweza  kutumika  kutengeneza  ndumba nzuri kutegemeana  na  nani  amelala  kwenye  kaburi  hilo.

Kwa  mfano  kwa  wale  walio fiwa  na  mama  zao  wazazi  na  wanataka  kutengeneza  ndumba  za  mapenzi, basi wanaweza  kutengeneza  uchawi  mkubwa  sana  wa  mapenzi  kwa  kutumia  mchanga  ulio  chotwa  kitaalamu kwenye  sehemu  ya  moyo  wa  kaburi  la  mama  ake  huyo. 

Sio hivyo tu, yapo  makaburi  ambayo  mchanga  wake  hutumika  kutengeneza  ndumba  ambazo  ni  tofauti  sana  na  dhana  iliyo jengeka  miongoni  mwa  watu  wengi  kuhusu  makaburi.

Kwa  mfano  kaburi  alilala  mtu  aliye  agwa  mara  mbili, kaburi  alilolala mtoto  wa  mwaka  mmoja na uchawi  katika  mapenzi, kaburi  alilo  zikwa  mtu ambae  msiba  wake  ulikaa  sehemu  mbili  tofauti ndani  ya  mji  mmoja , kaburi  alimo lala  marehemu  ambae  maiti  yake  iligombewa mahala pa  kuzikwa  nakadhalika.

Sasa  basi  mchanga  kutoka  kwenye  kaburi  alilo zikwa  mtu  aliye  tajirika  kupitia  kamali   hutumika  kutengeneza  uchawi  wa  kuwatajirisha  watu  kwa  njia  ya  kamali.

Kinyume  chake, kaburi  alimo zikwa mtu  ambae  alifilisika  kupitia  kamali,  mchanga  wake  hutumika  kutengeneza  uchawi  wa  kuwafilisi  watu, kuwatia  umasikini na  ufukara  pamoja  na  kuwafanya  watu  wenye  mali  nyingi  kufilisika  kwa   kuwekeza  pesa  zao  kwenye  biashara  zenye  risk kubwa.

Kwa  hiyo  kamali  ni  mchezo  unao  husisha  uchawi  na  ushirikina  kwa  kiwango kikubwa  sana.  Hii  ni kwa  sababu  kamali  ni  mchezo  wenye  pesa  nyingi  sana. Katika  ulimwengu  wa  kitabibu, kamali  haichukuliwi  tu kama  mchezo wenye  kuhusisha  bahati   ya  mtu, isipokuwa    huchukuliwa  kama  shughuli au  biashara  nyingine  yoyote  ile  yenye  kuleta  fedha  na  mali  nyingi  kama  vile biashara  ya  uchimbaji wa  madini nakadhalika.

Kwa  sababu  hiyo  basi  wacheza  kamali  wakubwa  wakubwa  wanapo  enda  kwa  waganga  kwa  ajili  ya  kupata  ndumba  za  kuwawezesha  kupata  mafanikio   kupitia  kamali  huwa  huwa  wanafanyiwa   ndumba  za  kuleta  mali  na  utajiri, kama  ambavyo  anaweza  kufanyiwa  mtu  ambae  anaingia  kwenye  biashara  ya  madini nakadhalika.

Hapa  nawazungumzia  wacheza  kamali  wanao cheza  mamilioni  ya  mapesa  kwenye  makasino  makubwa  na  ambao  kamali  ndio  chanzo  chao  kikuu  cha  mapato.

Kamali  ni  mchezo  wenye  ushindani  mkubwa  sana   ambao ndani  yake  unawahusisha  watu  wengi na  ambao  wengi  wao wanatumia  uchawi  kushindana.

Katika ulimwengu  wa  kitabibu  mcheza  kamali  huchukuliwa  kama  mtu  anae fanya  biashara  nyingine  yoyote  yenye  pesa nyingi  kama  vile  biashara  ya  uchimbaji  na  uuzaji  wa  madini  nakadhalika.

Na  hii ndio  sababu  kuu   wacheza  kamali  wanapo  enda  kwa waganga  kwa  ajili  ya  kupewa dawa za  kuwasaidia   kupata  mafanikio  katika  kamali  hupewa  ndumba  za mali  na  utajiri.

Mfano  pete  maalumu wanazo vaa  wacheza  kamali  ambao  watu  wengi  huziita  pete  za  bahati, si pete  za  bahati  kama  watu wengi  wanavyo  fikiri  isipokuwa  ni  pete    maalumu  za  majini  wa  mali na  utajiri.  Watu  wanao vaa  pete  hizo  wanakuwa  wameunganisha  nyota  zao  na  majini  hao  wa  mali  na  utajiri  ambao  huwasaidia  kuvuta  na  kupata mali  kwa  njia ya  mchezo  wa  kamali.

Hata  wale  wanao  chanjiwa ndumba maalumu  kwa ajili  ya  kamali, wengi  huchanjiwa  ngekewa  au  dawa  maalumu za  kuvuta  mali na  utajiri  ambao  huupata  kwa  njia  ya  kamali.

Mchezo  wa  kamali  ni  mchezo ambao  una  miiko  mingi  ambayo  wacheza  kamali  wengi  huifuata  na  kuiishi.

Ni mchezo  wenye pesa  nyingi  sana  ambao  unaweza  kubadilisha  maisha  ya  mtu usiku na  mchana. Na  kama  wasemavyo  wahenga, palipo na  riziki  hapakosi  fitina.

Hata wewe  unaetafuta  riziki nautajiri  kwa  njia  ya  kamali  unaweza  kufanyiwa  fitina  pia  na  wachawi.

Wachawi  wanajua  kuwa  kwenye  kamali  kuna  mamilioni ya  pesa na wanaweza  kukutupia  nuksi  itakayo  kufanya  usifanikiwe  kushinda  kamali  kwa  sababu  kwa  wao  wachawi  kamali  ni  shughuli  ama  biashara  nyingine  yoyote  ile.

Hata  hivyo, kamali  pia  ni mchezo  unao  weza  kumtia  mtu  umasikini  na  ufukara  ndani  ya  muda mfupi  sana.

Kwa Makala mbalimbali  kuhusu  ulimwengu  usio onekena, tembelea:

                www.mungwaherbalist.blogspot.com
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )