Monday, March 19, 2018

Ngara: Kijana Amuua Mama Mkwe Wake na Kumjeruhi Mke wake Kwa Mapanga


Kijana aliyefahamika kwa majina ya Joseph Medardi (32) mkazi wa Nyakahanga Wilaya ya Ngara mkoani Kagera amemuuwa mama mkwe wake Elizabeth Simon (70) kwa kumkata kata mapanga na kumjeruhi mkewe Elice Joseph (28) kisha na yeye kujimwagia petroleum.

Kijana huyo amefanya tukio hilo kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa na matatizo na mkewe kuhusu suala la unyumba jambo ambalo lilimpelekea kumrudisha mkewe huyo nyumbani kwa mama yake, ambapo amekaa huko takribani wiki tatu, siku moja kabla ya kikao cha kuwasuluhisha wanandoa hao ndipo kijana huyo ametekeleza mauaji hayo.

Mtoto wa marehemu Elizabeth Simon (70) ambaye ni Mchungaji Ezekia Simon amesimulia jambo hilo kwa undani zaidi na kusema kuwa chanzo cha yote hayo kuwa ni matatizo ya unyumba na kudai kuwa kijana huyo ambaye yeye ni shemeji yake alionekana amekuja na kusudio la kuwauwa wote yaani mama yake pamoja na mdogo wake huyo ambaye amejeruhiwa tu.

"Kisa cha kifo cha mama kimetokana na Mume wa dada kutoelewana katika habari za unyumba. Walikuwa na mgogoro kwa maana hiyo ikapelekea kumfukuza mkewe hivyo alikuja hapa yapata kama takribani wiki tatu yuko hapa nyumbani na baada ya hapo mimi kama Mkuu wa familia nilijaribu kutafuta njia ya kuwasuluhisha hivyo tarehe ambayo tulipanga kukutana ilikuwa jana ingawa hatukufanikiwa kukutana baada ya mzazi wa kijana kusema hakupata taarifa, matokeo yake yule kijana ndiyo amekuja akawashambulia mama pamoja na dada na kusababisha mauti ya mama" Alisema Mchungaji Simon  na kuendelea;

"Yule kijana alikuja kwa lengo la kuuwa wale na yeye kujiuwa kwa sababu alipowashambulia na kuwajeruhi yeye alijimwagia Petroleum na kujichoma moto ndani ya nyumba hii hii"
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )