Thursday, March 15, 2018

POLISI: Asiyejua kufa akachungulie kaburi

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi, CP Nsatu Marijan amesema hali ya usalama nchini imezidi kuimarika kwani hakuna tishio lolote la kiuhalifu linaloweza kutokea kwasababu Jeshi la Polisi limejipanga ipasavyo na halishindwi na chochote.

Kamishna Marijan ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anatoa salamu za kumuwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro katika uzinduzi wa vituo vidogo vya polisi vinavyo hamishika 'mobile Police Station' ambapo vitaanza kutumika katika mkoa wa kipolisi Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

"Jeshi liko imara, matukio ya uhalifu nchini yamepungua sana, hakuta tishio lolote ambalo lipo nje ya uwezo wa Jeshi la Polisi kushindwa kulikabiri. Sisi kama Jeshi la Polisi tutaendelea kuhakikishia nchi hii inaendelea kuwa salama ili wawekezaji na wananchi waweze kufanya shughuli zao bila ya taflani yeyote", amesema Kamishna Marijan.

Pamoja na hayo, Kamishna Marijan ameendelea kwa kusema "kama mtu ana wasiwasi na Jeshi letu basi ajaribu kufanya lolote maana wanasema asiyejua kufa basi akachungulie kaburi. Sisi tupo imara tutaendelea kuwa imara".

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema vituo hivyo vilivyo zinduliwa leo vitatumika kwa kadri ya maelekezo ya maeneo yenye uhalifu utakapotokea eneo fulani na endapo utapungua basi watavihamishwa na kwenda eneo jingine lenye uhalifu.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )