Sunday, March 4, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Ishirini ( 20 )

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOSIHIA

   Nikanyanyuka kwenye kiti kwa hasira na nikapiga hatua za haraka kumfwata Hilda sehemu aliyo simama  na akaanza kukimbia kuelekea ndani kwangu huku na mimi nikimkimbiza kwa nyuma na kabla hajashika kitasa cha mlango wa kuingilia chumbani kwangu akakanyaga maji yaliyopo juu tarzi na gafla akateleza na kuanguka kwa kwa nyuma na kichwa chake kikapiga chini kwa nyuma na damu zikaanza kusambambaa taratibu kutoka sehemu kilipo angukia kichwa cha Hilda na kuufanya mwili wangu kuanza kutetemeka kwa woga

ENDELEA
   Nikamsogelea Hilda na kukuta akirusha rusha miguu yake kama mtu anaye kata roho na kuzidi kunichanganya huku jasho jingi likianza kunitoka mwilini mwangu.Nikasimama kwa muda nisijue nini cha kufanya nikapiga hatua za haraka na kuingia jikoni na kuanza kutafuta kitu nisicho jua,Kwa kuchanganyikiwa nikajikuta nikizunguka jikoni zaidi ya dakika kumi huku kila ninacho kishika kwangu ninakiona ni kibaya.Nikachukua kitambaa cha kukaushia vyombo baada ya kuoshwa kisha nikatoka nacho hadi sebleni.Mapigo ya moyo yakazidi kunidunda kiasi kwamba hadi sauti ya mapigo ya moyo nikaanza kuyasikia yakidunda kwenye kifua changu hii ni baada ya kuto na kutokuuta mwili wa Hilda zaidi ya kuona michuruziko ya damu inayo elekea mlango wa kutokea nje

    Nikajishauri kwa muda kisha taratibu nikaanza kupiga hatua za taratibu kuelekea mlango wa kutokea nje na kabla sijaufungua mlango wa mbele ambao umefugwa na funguo kama Halda alivyo ufunga nikaamua kurudi jikoni huku akilini nikiwaza kwenda kuchukua kisu kwa ajili ya kujilinda kwa chochote kitakacho jitokeza mbele yangu.Nikanza kusogeza kitu kimoja baada ya kingine nikitafuta kisu na sikukiona kwa haraka nikachukua uma wa kulia chipsi na kutoka huku mkono mmoja nikiwa nimeshika kitambaa ambacho sikujua nitakitumia kwenye nini.Nikafungua kwa tahadhari  mlango wa nje na kuchungulia na sikuona kitu chochote zaidi ya gari la Hilda

    Nikaanza kujiuliza ni wapi mwili wa Hilda emekwenda na mbaya michuruziko ya damu imeishia katika mlango wa kutokea nje .Nikageuka na kuufungua mlango na kuingia ndani huku akili ikiwa imevurugika nikapiga hatua za taratibu na kukaa kwenye mguu wa sofa kabla makalio yangu hayajafika kwenye mguu wa sofa taa zote za nyumbani kwangu zikazimika na nikajikuta nikisimama wima kama askari anaye subiria wimbo wa taifa lake.Gafla nikasikia watu wawili sauti ya kiume na yakike zikibishana chumbani kwangu na kujikuta nikizidi kutetemeka kwa woga huku mwili wangu ikinisisimka na vinyweleo vyote vikanisimama.

   Mabishano ya watu hao yakazidi kupamba moto huku mwanamke mwenye sauti kama Hilda akimuomba mwanaume huyo asitoke nje ila mwanaume anang’ang’ania kutoka.Akili yangu kwa haraka ikarudisha kumbukumbu ya mazungumzo ya bibi kuwa Hilda ni mke aliye olewa na jini lililopo kifungoni na sikujua kama ndio lenyewe linalo bishana au kuna jingine.Mwili mzima ukazidi kusisimka huku ukitetemeka na gafla nikastukia nikishikwa begani na kitu chenye mkono wa baridi kiasi kwamba hata kama umevaa jaketi baridi yake ni lazima ipeye kwenye mwili wako

Nikajua tayari nimekwisha na taratibu nikageuka huku nikiwa nimeyafumba macho yangu ili nisione ninacho kwenda kuonana nacho,Nikastukia kikinigusa  shavuni kwa mkono wake wa baridi na kujikuta nikizidi kutetemeka kwa woga na kwa mbali nikaanza kuyafumbua macho yangu na nikajikuta nikizidi kuyafumbua kwa mshangao kiasi kwamba ninajikuta nikimeza fumba kubwa la mate kulisuuza koo langu ambalo limekauka

“Rahma”
Niliita kwa sauti ya chini huku nikitazamana na Rahma ambaye amesimama mbele yangu huku akiwa amevalia gauni jeusi kama anakwenda msibani
“Shiiiiii”
    Rahma alikiweka kidole chake mdomoni akiniashiria nisizungunze kitu cha aina yoyote na kunifanya nikae kimya huku nikijiuliza maswali imekuwaje kuwaje hadi Rahma ametokea sehemu hiyo.Akanishika mkono na taratibu tukaanza kupiga hatua za kutoka nje huku macho yangu nikiwa nimeyaelekeza mbele na sikutaka kutazama nyuma na laiti kama nitasikia mlio wowote miguu yangu imejiandaa kwa kazi ya moja tuu ambayo ni kukimbia kuyaokoa maisha yangu

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )