Saturday, March 10, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Ishirini na Sita ( 26 )

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

“Anaitwa nani?”
“Anaitwa RAHMA anasoma kidato cha nne”
Nikajikuta nimekaa kimya nikimtazama mkuu wa shule huku nikijiuliza kama akili zake zinafanya kazi sawa sawa au ndio uzee unamchanganya

ENDELEA
Nikakaa kimya huku nikimtazama mkuu wa shule machoni kwani sikujua ni nini nimuambie
“Eddy ukihitaji hata pesa mimi nitakupatia ili tu nimpate Rahma”
“Ila mkuu mbona msichana mwenyewe simuoni hapa shule”
“Amesafiri ila akirudi tu nataka niweke mambo sawa”
“Usijali mkuu wangu”

Nikajikuta nikinyanyuka kwenye kiti nilicho kaa na kumuaga mkuu wa shule na kumuahidi nitalifanyia kazi na nikarudi ofisini kwa waalimu wengine na kuwakuta kila mmoja akiendelea na shuhuli yake kutokana sikuja kikazi nikabaki nikiwa ninajisomea baadhi ya vitabu vinanavyohusiana na masomo yangu ninayo yafundisha.Simu yangu ikaingia ujumbe mfupi wa meseji na nikakuta ni namba ya Rahma
“BABY UWAHI KURUDI NIPO NYUMBANI KWAKO NA HALDA”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio baada ya kuona saa ya kwenye simu yangu inaonyesha zimabaki dakika kumi kutimu saa sita kamili kabla haujafika muda tulio ahidiana na mchungaji juu ya kwenda kufanya mamombi ambayo kwa wakati huu kwangu sikuyaona na umuhimu wa aina yoyote kwani mchungaji mwenyewe anaushirikiano na Olvia Hitler.Nikanyanyuka kwa haraka na kabla sijaufikia mlango wa kutokea ofisini simu yangu ikaita na kuikuta ni namba ya mchungaji,nikabaki nikiitazama pasipo kuipokea na kumfanya madam Recho kuzungumza

“Jamani si mzime misimu yenu inatupigia kelele”
Niakageuka na kumtazama madam Recho na sikuseme kitu cha aina yoyote zaidi ya kuminya kitufe cha kupokelea simu na kuiweka sikioni na kuisikia sauti ya mchungaji
“Mpendwa tumefika nyumbani kwako tupo hapa getini tunaomba utufungulie mlango kwa maana tunapiga honi nahisi uisikii kutokana na mziki ulio ufungulia kwa sauti ya juu”
“Ahh...Sawa mchungaji nakuja”
Nikakata simu na kubaki nikiwa nimetizama chini huku nikishush pumzi na sikujua nifanye nini kuhusiana na swala la kwenda nyumbani kwa kwangu kwani hali ya hewa imesha haribika.

“Eddy unapakwenda?”
Mkuu wa shule aliniuliza na nikamjibu kwa kutingisha kwichwa nikiashiria kuwa sina pa kwenda
“Basi twende sehemu moja kama huto jali”
“Sawa mkuu”
Tukatoka ofisini na kuingia kwenye gari ya mkuu wa shule na sikujua ni wapi tunakwenda na ndani ya gari sikuzungumza kutu cha aina yoyote hadi tukafika kwenye moja ya mtaa ambao sikuujua jina lake na sote tukashuka kweye gari na mkuu wa shule akaminya kengele ya getini kwenye nyumba nzuri na baada ya muda geti likafunguliwa na akatoka msichana mdogo anaye onekana ni mfanyakazi wa ndani na baada ya kumuona mkuu wa shule akaanza kumchangamkia huku wakitaniaana kwa baadhi ya maneno kisha akatukaribisha ndani na moja kwa moja tukapitiliza hadi sebleni na tukakaa kwenye sofa na msichana wa kazi akasimama na kuiwasha tv iliyopo ukutani na kuaanza kuadilisha badilisha chaneli zilizopo kweye king’amuzi wanacho kitumia

“Babu siku hizi mambo yako sio mabaya naona dada akakupendezesa ana”
“Kawaida babu yangu”
“Mmmm kweli ni kawaida kwani hiyo inye uliyo ifungashia utaweza kusema kuwa wewe ndio mwenye nyumba”
“Babu jamani hujaacha vituko vyako?”
“Ndio ukweli na siku hizi unanga’aa sana”
“Asante”
“Haya huyu mwenzako yupo wapi?”
“Dada amekwenda hospitalini mara moja ila muda si mrefu atarejea”
“Ahaa amakwenda hospitali gani?”
“Buriani”
“Eddy hapa ni nyumbani kwa  madam Rukia”
“Ahaaa asante”
Mfanyakazi wa ndani akaondoka na kwenda jikoni na kutuacha tukia tunatazama Tv baada ya muda kidogo mkuu wa shule akanyanyuka na kuniambia anakwenda mara moja jikoni kuzungumza na mfanya kazi wa ndani.Nikabaki nikitazama Tv galfa nikasikia simu yangu ikiita na nikaitoamfokoni na kuikuta ni namba ya mchungaji,Sikutaka kuipokea nikaiweka simu pembeni huku nikitafakari ni kitu gani nifanye.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )