Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, March 7, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Ishirini na Tatu ( 23 )

adv1
AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Mchungaji akazidisha sauti ya kuomba na kila anvyozidi kuomba ndivyo jinsi hali ya hewa ikazidi kubadilika ndani ya nyumba hadi ikafikia hatua nikaanza kuogopa.Upepo mkali unaokwenda mithili ya kimbuka kikali ukaanza kuzunguka sebleni na baadhi ya vitu vikaanza kuanguka chini ikiwemo vyombo vilivyopo ndani ya kabati.Nikastukia nikamuona Joseph akirushwa na kupiga ukutani na akatulia kimya na gafla nikamshugudia mchungaji akichomwa na kisu kilichoruka kutoka kabatini na kikatua kifuani kwake

ENDELEA
Mchungaji akakishika kishu kilicho mchoma na kukichomoa na kuzidi kuomba huku akiiongeza sauti ya juu huku akiliitaja jina la Yesu kristo.Miale ya radi na kurumo ikanza kupiga maeneo ya dari na kusababisa nilale chini kwa woga ila mchungaji hakulala chini na akazidi kuomba na taratibu na mimi nikajikuta nikiisema

“SHINDWA KATIKA JINA LA YESU KRISTO”
Nikaendelea kurudia rudia maneno hao mara gafla nikajikuta nikinyamaza baada ya Olvia Hitler kusimama kwenye moja ya kona huku akiwa amevalia nguo nyekundu na sura yake ikiwa imejawa na hasira kali sana kiasi cha macho yake kutoa mwanga mkali
“Wewe pepo unayetaka kuchukua watu wa bwana leo hii ndio mwisho wako nakufunika na kukurudisha kuzimu katika jina la YESU KRISTO wa nadhareti TOOKKKKAAAAAAAAAAAAAAA”
Olvia Hitler akayumba kidogo akionekana kama ametetemeshwa kwa maneno hayo ila akanitazama kwa macho makali na kuninyooshea mkono na kujikuta nikikabwa shingo na kitu nisicho kiona na taratibu nikaanza kunyanyuliwa kwenda juu.Mchungaji akaunyoosha mkono wake mmoja kwangu huku akiomba kwa nguvu na kujikuta nikianguka chini na gafla Olvia akapotea na hali ya ndani ikaanza kutulia na baada ya muda ikarudi katika hali ya kawaida ila vitu vingi vimechanguka na kukaa katika sehemu tofauti na nilivyokuwa nimevipanga

Mchungaji akasogea taratibu na kukaa kwenye sofa huku jasho jingi likimwagika na nikaonda shati lake likilowana na damu
“Mchungaji umeumia hapo kwenye kifua”
“Hakuna tabu ni jeraa dogo ila tafuta maji na chumvi unilete hapa”
Nikatoka kiwoga woga na kwenda jikoni na kuanza kuitafuta  chumvi na baada ya muda nikaipata kisha nikaweka maji kwenye kikombe na kurudi sembeni.Mchungaji akavichanganya kwa pamoja maji na chumvi kiasi akaviombea na kujipaka kwenye jeraha lake na kuifanya damu kuacha kutoka.Akasimama na kumshika Joseph kichwani na kuanza kumuombea taratibu hadi Joseph akapia chafya na kunyanyuka.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )