Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, March 21, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Sita ( 36 )

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

“Hujui kuwa wewe ndio chanzo cha haya yote”
Nikabaki nikiwa ninamtazama Rahma huku nikikosa la kunzungumza na sikjua nimwambie nini juu ya kitu anacho dai mimi ni chanzo

ENDELEA
“Rahma unaposema kuwa mimi ni chanzo sijakuelewa una maana gani?”
“Eddy tambua ya kuwa kila ulilolkuwa ukilifanya haya ndio matokeo yake”
Moja kwa moja nikaanza kuhisi Rahma ameingundua tabia yangu ya zamani,ikanibidi niibadilishe mada kuepukana na mizozo ya kelele.
“Fanya basi upike msosi baby ninanjaa?”
“Sawa mume wangu ila hiyo mada tutazungumza baadaye vizuri”

“Mume wangu unanichekesha sana”
Rahma alizungumza nyuma yangu na kunifanya nigeuke na kumtazama
“Kwa nini?”
“Kwa maana wewe unajing’ang’aniza kupanda juu ya huo mti wakti unauona ni mkubwa na tangu kule ndani niliikuwa nikikuangalia jinsi unavyo paramia parami”Rahma alizungumza huku akicheka

“Kinacho kuchekesha wewe haswa ni nini?”
“Ninakucheka wewe unaye nga’angana kuapanda hapo”
Nikamtazama Rahma kwa macho ya umakini na kujikuta nikiachia msunyo ulio mnyamazisha kuchela
“Baby jamani mbona unanisunya?”
“Nenda ndani kaniletee maji ya kunywa”
“Sawa mume wangu au umechukia nilivyo kucheka?”
“Hapana”
Rahma akanisogelea na kunibusu shavuni na kuondoka kwa mwendo wa madoido,Sehemu niliyo simama nikaanza kuhisi mtetemeko ulio nifanya nitazame chini kwa muda.Nikajaribu kupakanyaga nikasikia mlio unao ashiria chini yangu kuna shimo.Nikaanza kuyasogeza majani mengi ya mti yaliyo kauka na nikakuta mfuniko ulio tengenezwa kwa chuma na niimara sana na juu yake ukiwa na mnyororo chakavu ulio unganika kwa pamoja

“Kuna nini hapo?”
Rahma aliniuliza huku akiwa ameshika jagi lenye maji pamoja na kikombe
“Humu ndani sijui kuna nini,ila ninahisi kuna viu muhimu sana”
“Mmmmm hembu”
Rahma akapiga hatua hadi sehemu niliyopo mimi na akanyaga mfuniko kama nilivyo ukanyaga mimi kwa kutumia mguu kisha akanitazama machoni.
“Baby iseje kukawa na madudu ya ajabu ikala kwetu?”
“Madudu gani?”
“Madudu tuu ya ovyo ovyo”
“Hakuna kitu.....Fanya hivi nenda kule jikoni kalete kile kijishoka kilicho ning’inizwa pale ukutani"
“Sawa”

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )